Home Uncategorized GAVANA TUTUBA: DIB IMEWEKA UTARATIBU MZURI KUREJESHA FEDHA ZA WATEJA

GAVANA TUTUBA: DIB IMEWEKA UTARATIBU MZURI KUREJESHA FEDHA ZA WATEJA

DODOMA

Gavana  wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Tutuba, amesema kuwa Benki hiyo kupitia Bodi ya Bima ya Amana (DIB) wameweka utaratibu mzuri wa kurejesha fedha za wateja kama ikitokea Benki imefilisika.

Amese kuwa Serikali imekuwa ikitekeleza jukumu la kuhakikisha wateja wote waliojitokeza wanarejeshewa fedha zao kulingana na kiwango cha Bima pamoja na kuwafatilia wateja wote waliokopa ili waweze kurejesha madeni yao.

Amesema kuwa DIB imeongeza kiasi cha urudishaji wa fedha kwa wateja kutoka milioni moja hadi milioni saba na Laki tano, wakiwa na lengo la kulinda amana ya mteja.

“Kiwango cha mikopo chechefu imeshuka hadi kufikia asilimia 4.3 ambacho ni kiwango kipo chini na ukilinganisha na utaratibu wa kimataifa”
Gavana Tutuba.

Katika hatua nyengine amewakumbusha
watanzania ambao walikuwa wanahifadhi fedha Benki ambapo kwa sasa Benki hiyo imefilisika, kwenda Ofisi ya DIB kwa ajili kuchukua fedha zao kama bado hawajazichukua. 

Previous articleDIB NA MKAKATI KABAMBE WA KUTOA ELIMU YA KWA USALAMA WA FEDHA KWA WANAWANCHI
Next articleWAZIRI JAFO ATEMBELEA BANDA LA TMDA NANE-NANE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here