Home BUSINESS EWURA YATETA NA MAJAJI,MAHAKIMU KUHUSU UDHIBITI

EWURA YATETA NA MAJAJI,MAHAKIMU KUHUSU UDHIBITI

Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji na mahakimu wa Mahakama ya Tanzania na watendaji wa EWURA baada ya kupata elimu kuhusu masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji, katika semina iliuofanyika Kituo Jumuishi cha Haki Jinai, jijini Dodoma leo 16/8/24.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo, 16/8/24 imekutana na majaji na mahakimu wafawidhi 50, katika semina ya kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa shughuli za kiudhibiti kwenye sekta za nishati na maji na usafi wa mazingira, katika kituo jumuishi cha Haki Jinai, jijini Dodoma.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, amewashukuru viongozi hao kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa EWURA katika utekelezaji wa majukumu yake na amewaomba kuendeleza ushirikiano huo.

Bw. Kaguo, pamoja na mambo mengine, alieleza changamoto kubwa ambayo EWURA inapata ni mahakama za chini kushughulikia kesi za kiudhibiti jambo ambalo baada ya majadiliano, ilionekana ni kinyume na misingi iliyopo kwa chombo hicho kutoa uamuzi kwa masuala ya kiudhibiti.

Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu nchini, Jaji John Kahyoza ameipongeza EWURA kwa utendaji mzuri na kushauri elimu iliyotolewa kwao kuwa endelevu na iwafikie watu wote.

”Tufikishieni salamu zetu kwa Mtendaji Mkuu, tumefurahia elimu hii na niwasihi muongeze kasi ya kuwafikia pia mama zetu na baba zetu kule vijijini, nasi tunaahidi kuwa mabalozi wenu”. Alisema

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo akitoa elimu kwa waheshimiwa na mahakimu wa Mahakama ya Tanzania, katika semina iliyofanyika Kituo Jumuishi cha Haki Jinai, jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji wakati wa semina iliyotolewa na EWURA kwa waheshimiwa majaji na mahakimu iliyofanyika jijini Dodoma leo 16/8/24

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here