Home LOCAL DCEA YAADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI JIJINI ARUSHA

DCEA YAADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI JIJINI ARUSHA

Na; Prisca Libaga, Arusha.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Asasi ya Youth Hub Arusha tarehe 12.08.2024 imeadhimisha Siku ya Vijana Duniani kwa kutoa elimu kinga kwa vijana 63 katika Ukumbi wa MS Training Center for Development Cooperation uliopo Leganga wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha. 
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 ni _”Vijana na Matumizi ya Fursa za Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu”_.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini pia ilitumia jukwaa hilo adhimu katika kuwahimiza vijana kutokujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya sababu vitendo hivyo vinaweza kukatisha ndoto zao.  
Vilevile iliwahamasisha vijana walioshiriki maadhimisho hayo kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.
Share this Article

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here