Mkuu wa Kitengo Mawasiliano na Mahusiano ya nje, Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Asumpta Muna, akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea katika Banda la BoT kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane-nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM
Chuo cha Benki Kuu kilichopo Jjini Mwanza, kimeendelea kutoa elimu kwa wananchi na makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wanaotembelea Banda la Benki Kuu katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane-nane, yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano ya nje wa Chuo hicho Bi. Asumpta Muna amesema kuwa chuo hicho kinatoa fursa kwa vijana wenye maono ya kufanya kazi kwenye sekta na taasisi mbalimbali za fedha. Â
Ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga pia kuwajenga wanafunzi kwenye maadili ili kuhakikisha wanawapata watendaji wazuri watakaosimamia suala zima la maadili katika sekta ya fedha.
Sambamba na hilo pia amesema kuwa Chuo hicho kina majumu ya kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wafanyakazi ili kuzidi kuwajengea uwezo na ujuzi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amefafanua kuwa Kutokana na mafunzo hayo kuwa mahili yamevutia nchi mbalimbali za jirani ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Msumbiji, Ghana, Malawi na Zambia, nakwamba zimekuwa zikileta wataalamu wao kupata mafunzo katika chuo hicho.
Aidha amesema kuwa Programu nyingine ni Stashahada ya uzamili (Postgraduate Diploma in Bank Management), mafunzo hayo yanayoendeshwa katika vyumba vya mafunzo vilivyopo Benki Kuu makao makuu ndogo Dar es Salaaam.
Sifa za kujiunga na programu hii ni Shahada ya kwanza (Bachelor degree), au Stashahada ya juu (Advanced Diploma) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali