Na: Hughes Dugilo, DODOMA
Afisa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Gabriel Girangay, mesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wakulima nchini kusajili alama za Biashara zao ili kuilinda bidhaa zao na kuwawezesha kutanua wigo wa masoko ya mazao yao nje na mipaka ndani ya nchi.
Girangay ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema kuwa wakulima kilimo ni sekta kubwa kwani imeajiri Watanzania wengi nakwamba wakulima wanapaswa kuelimishwa umuhimu wa kusajili alama za Biashara zao, kwani hatua hiyo itawanufaisha zaidi katika kufanya Biashara.
“Tuko kwenye maonesho haya ya Nanenane kwa ajili ya kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya kilimo na wananchi wote kwa ujumla, kizingatitia kuwa Wakulima ni wadau muhimu sana kwani ndiyo maana tuko hapa kutoa elimu watambue umuhimu wa kulinda bidhaa zao. ” amesema Girangay.
Ameongeza kuwa katika maonesho Hayo wapo wataalamu ambao wanakutana na wananchi na na kuwaelimisha juu ya majukumu yao, na kutoa huduma za papo kwa hapo ikiwemo Leseni ya Biashara.
“hapa katika Banda letu tunatoa huduma za kusajili jina la Biashara na kila Mtanzania mwenye nia ya kuanzisha Biashara afike kwani kuna wataalamu wa sekta mbalimbali wanaotoa huduma kwa njia ya mtandao na kumuwesha mteja kupata Leseni yake papo hapo” ameongeza.