Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi Sekta ya Fedha, Idara ya huduma ndogo ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Deogratius Mnyamani, akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa Habari katika maonesho ya N
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wakulima katika kuhakikisha wanapata mikopo kwa riba nafuu ili waweze kufikia malengo na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza kwenye mahojiano katika Maonesho ya kimataifa ya kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi Sekta ya Fedha, Idara ya huduma ndogo ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Deogratius Mnyamani, amesema kuwa BoT imetenga fedha kwa ajili ya taasisi za fedha ikiwemo mabenki ili waweze kuwakopesha wakuilimo kwa riba nafuu.
Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mikopo kwa gharama nafuu ili kuleta tija kwa Taifa katika sekta ya kilimo.
Amesema kuwa ili mkulima apige hatua katika mafanikio anatakiwa kuwa mipango pamoja na kufanya uwekezaji katika sekta ya kilimo jambo ambalo litaleta tija na kufikia malengo husika.
Amesisitiza kuwa taasisi za fedha zinapaswa kutoa mikopo kwa wakulima kwa kuzingatia riba nafuu ili kuhakikisha malengo yanafikiwa.
“Pia kuna fursa mbalimbali kwa wale ambao wanataka kuanzisha biashara za huduma za fedha katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini kwa kuwakopesha wakulima wadogo”