Mwita Patrick Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la BoT ili kupata elimu ya fedha kwenye banda la BoT katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina akimkabidhi zawadi mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.
Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina pamoja na Mariam Kopwe kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT wakiwa kwenye banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.
Geofrey Jonas Valonge Afisa wa Benki Kuu BoT kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki kushoto na Francis Mdoe Afisa wa Benki Idara ya Huduma za Kibenki BoT Dodoma wakiwaonesha noti halisi na noti bandia baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo.
(PICHA NA: HUGHRS DUGILO)
Na; Hughes Dugilo, Dodoma.
Benk Kuu ya Tanzania BoT imetoa elimu kwa wananchi kupitia maonesho ya kilimo ya kimataifa Nane-nane yanayoendelea katika viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma.
Akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo, Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania Mwita Patrick amesema mwaka huu kuna makadirio ya ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.4 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo uchumi ulikuwa kwa asilimia 5.1.
“Sisi watu wa sera ya fedha tunajukumu la kuhakikisha fedha zilizoko kwenye mzunguko zinachangia kufikia malengo ya kuwa na mfumuko wa bei ambao uko ndani ya wigo wa asilimia 3 na 5”, amesema.
Aidha, amesema wana majukumu mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kutoa takwimu za kiuchumi, kufanya tafiti za masuala ya fedha na uchumi, pamoja na kuandaa ripoti mbalimbali za kiuchumi.
Pia amesema kuwa BoT inaweza kuwakopesha mabenki ya biashara kwa muda maalumu, nakwamba endapo kunatokea kuwepo na ongezeko la fedha wanalazimika kuziondoa kwenye mzunguko kupitia nyenzo mbalimbali za Sera ya Fedha.
“Kwa sasa riba ya Benki Kuu ni asilimia 6 kwa robo mwaka ya tatu ya mwaka 2024, kama ilivyokuwa katika robo ya pili. Hii ni kutokana na kupungua kwa viatarishi mbalimbali vya kiuchumi ikiwemo tishio la mfumuko wa bei na kuendelea kuimarika kwa mazingira ya uchumi wa Dunia.