Home BUSINESS WAZIRI BASHE ATANGAZA NEEMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KATAVI

WAZIRI BASHE ATANGAZA NEEMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KATAVI

* Serikali yawekeza zaidi ya shilingi Bilioni 55 Katavi

* Azindua ujenzi wa Maghala mawili na kuweka Jiwe la Msing ujenzi wa Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji

* Aishukuru Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kutekeleza miradi zaidi ya 29 mkoani Katavi

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ametangaza neema kwa wakulimo wa Mkoa wa Katavi na kusisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kwa zaidi ya shilingi Bilioni 55 mkoani humo.

Waziri Bashe ametangaza neema hiyo katika kijiji cha Mwamkulu, wakati wa akizindua ujenzi wa maghala mawili na kuweka Jiwe la Msing la Ujenzi wa Ukarabati wa Skimu ya Umwagiliaji.

Ametumia fursa hiyo kusifu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) chini ya Uongozi wa Bw. Raymond Mndolwa kwa kutekeleza miradi zaidi ya 29 katika Mkoa wa Katavi.

Waziri Bashe amesema kuwa lengo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuujengea uwezo mkoa wa Katavi na nchi nzima kwa ujumla, ili kuzalisha chakula cha kutosha cha kulisha ndani na nje ya nchi litafikiwa kutokana na uwekezaji huo mkubwa unaoendelea.

“Naomba kuwasilisha salamu za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anaahidi kuja kushiriki katika uzinduzi wa miradi mingine ya Umwagiliaji katika Mkoa huu wa Katavi, ikiwemo Kata ya Mwamkulu kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao,” amesema Waziri Bashe.

Waziri Bashe pia amewaasa wakulima wa Mwamkulu kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji ulianzishwa kwa ajili ya kuwezesha wakulima kuchangia kufanya marekebisho ya miundo mbinu na kuchangia kujenga maeneo mengine. Pia ametoa wito kwa wakulima kupata haki ya kumiliki maeneo yao kisheria kwa kuwa maeneo ambayo Serikali imewekeza lazima yalindwe.

Waziri bashe amebainisha kuwa Makubaliano ya Serikali ni kujenga miundombinu katika hekta 27000 kwa wilaya zote mbili na kwamba imeanza na hekta 6000. “Malengo ya Serikali ni wakulima muweze kulima mara mbili hadi mara tatu kwa mwaka,” alisema Mhe. Bashe.

Bashe amebainisha kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji na kuwa pamoja na uwekezaji huo, mashamba yanayowekewa miundombinu yataendelea kuwa mali ya wananchi.

“Kuna skimu zitafanyiwa utekelezaji ambazo ni skimu za Itenka 4500, kakese 3000, karema zaidi ya hekta 5000. Hekta zote 25000 zitangazwe mwaka huu,” amesema Waziri Bashe, huku akielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutangaza kwa wakati.

Previous articleWAZIRI BASHE AKIKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI SKIMU YA USENSE
Next articleBASHE: MSIUZE MASHAMBA, TUNZENI ARDHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here