Home BUSINESS WAZIRI BASHE AKAGUA MIRADI SKIMU YA UMWAGILIAJI, MWAMKULU KATAVI

WAZIRI BASHE AKAGUA MIRADI SKIMU YA UMWAGILIAJI, MWAMKULU KATAVI

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameongoza ukaguzi wa miradi ya skimu ya umwagiliaji ya Mwamkulu, Mkoani Katavi tarehe 19 Julai 2024 katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Waziri Bashe ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuf kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi; na Bw. Raymond Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukagua ujenzi wa mifereji, ofisi ya Meneja wa mradi wa ujenzi na ukarabati skimu ya umwagiliaji ya Mwamkulu, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo na ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhia mchele, no mpunga na mashine ya kukobolea mpunga.

Mradi huo upo katika kijiji cha Mwamkulu, mkoani Katavi. Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamkulu ina ukubwa wa hekta 3000 ambazo zitanufaisha wakulima takribani 20,000.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here