Home BUSINESS TTCL KUPELEKA T – CAFE KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU

TTCL KUPELEKA T – CAFE KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU

 Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam 

SHIRIKA ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imekuja na huduma mpya ambayo itahusisha kufunga mtandao kwa bei nafuu katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama Vituo vya, Treni, Viwanja vya Ndege na vituo vya Mabasi inayojulikana kama (T-CAFE).

Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL Bi. Zuhura Muro amesema Shirika hilo linatekeleza mradi huo ili kuwawezesha watu mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara, Waandishi wa habari na watu wote ambao mara nyingi shughuli zao huzifanya nje ya ofisi zao watatumia maeneo hayo kutekeleza.

 

“Tumekuja na mradi mwingine wa kutoa huduma katika maeneo ya mkusanyiko ya watu (Public WIFI) ambapo huduma hii itapelekwa katika Vyuo Vikuu, maeneo yenye mkusanyiko wa watu na sasa tumekuja na bidhaa mpya inaitwa T-CAFÉ”
 
 
Huduma hii pamoja na mambo mengine shirika litashirikiana na watoa huduma nyingine mfano wauzaji wa kahawa ili kuwezesha wateja wakati wakiendelea na kazi zao kimtandao basi wananweza kupata kitu chochote cha kula au kunywa hivyo shirika linaamini huduma hii itakuwa suluhisho la walengwa kutimiza majukumu yao kwa wakati na kutimiza malengo waliyojiwekea.
 
 
Akizungumzia kuhusu ushiriki wao katika maonesho ya saba saba mwaka huu Bi. Zuhura alisema ushiriki wa TTCL unaenda sambamba na kauli mbiu inayosema ‘Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji’ na kwamba kama shirika hilo lina wajibu mkubwa kufanya biashara kwakuweka mazingira mazuri ya kufanya uwekezaji.

 

 

 

 

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani tayari inaendelea kufungua milango mingi ya kiuchumi na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kuvutia uwekezaji hivyo TTCL inao wajibu mkubwa wa kuhakikisha huduma ya intaneti na mawasiliano inakuwa katika hali bora ili kuwawezesha Wafanyabiashara na Wawekezaji kufanya shughuli zao kidigitali.
 
 
‘‘Kutokana na kauli mbiu hii basi sisi tumejipanga kama shirika katika mikakati ambayo itawezesha wanaowekeza Tanzania kutoka nje na ndani ya nchi kuweza kuungana na dunia kidijitali uwe mahali popote unaweza kuunganishwa kidijitali kutokana na nguvu ya mawasiliano TULIYONAYO, “amesema Bi Zuhura.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here