Shirika la utafiti na Mendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) linashiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Dar Es salamaa maarufu kama Sabasaba limesema Matumizi bora ya nishati ni muhimu katika maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla kiuchumi, kimazingira na kudumisha afya bora za watumiaji wa Nishati safi ya kupikia
Akizungumza katika banda la TIRDO kwenye maonesho hayo Mhandisi Augustino Masse ameelezea kuwa Umuhimu wa utunzaji wa mazingira na afya bora unaathiriwa sana na nishati isiyo safi, hasa mkaa utokanao na miti. Matumizi bora ya nishati kwa ufanishi ni hamasa inayotolewa kwa watanzania wote ili kubadili matumizi ya nishati iliyozoeleka ambayo ni mkaa wa miti na kuanza kutumia mkaa utokanao na mabaki ya mazao ya kilimo na nyinginezo kama gesi asilia.
Amesema Ili kuyafikia matumizi ya nishati safi ya kupikia; elimu ya matumizi ya nishati safi ni muhimu kwa watumiaji, inatakiwa ikiwa ni pamoja na ubora wa majiko yaliyo na ufanisi zaidi ya majiko ya mafiga matatu ufikiwe, pamoja na nishati tunazotumia ziwe safi kwa mazingira na watumiaji.
Mhandisi Augustino Masse ameongeza kuwa Matumizi bora ya nishati kwa ufanisi viwandani na majengo makubwa. Viwanda ni chachu ya maendeleo ya kila taifa lilioendelea duniani.
“Nishati nyingi hasa ya umeme hupotea viwandani bila wenye viwanda kujua. Kwa kupunguza upotevu wa nishati viwandani tunaweza kuhudumia wananchi wengi zaidi hasa kule ambako umeme haujafika. ” Amesema Mhandisi Augustino.
Amesema hatua za kufikia matumizi bora ya nishati kwa ufanisi ni
Kuelewa jumla ya matumizi yako ya nishati na mgawanyiko wake kiwandani au kwenye jengo,
Fanya ukaguzi wa mifumo ya matumizi ya nishati ili kujua sehemu zinazosabalisha na kuleta upotevu,
Ameongeza kuwa ni muhimu kuandaa mpango mkakati wa kupunguza upotevu wa nishati, ukianza na kubadili tabia ya watumiaji, Kutekeleza mpango wa kuzuia au kupunguza upotevu wa nishati,
Kufuatilia na kujua kiwango cha nishati ambacho kimezuiwa kupotea na mikakati iliyotekelezwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuboresha mikakati ya kuokoa nishati kwani zoezi hili hua ni endelevu.
Mhandisi Augustino Masse amesema kuwa, Ili kuhakikisha ubora wa malighafi, bidhaa, miundombinu na mitambo, ukaguzi unatakiwa kufanyika kila baada ya muda fulani kulingana na matumizi ya kitu husika.
Ameongeza kwamba Kuna bidhaa, miundombinu, malighafi na mitambo ambayo inatakiwa kufanyiwa ukaguzi na kuendelea kufanya kazi, hivyo basi ukaguzi usioleta uharibifu au kubadilisha uwezo wa utendaji kwa kitu husika unahitajika.
Ameongeza kuwa TIRDO inatoa huduma hiyo kwa njia kuu tano ambazo ni mahususi kugundua hali ya kitu kinachochunguzwa. Njia hizo ni 1 ukaguzi wa kitaalamu wa kuangalia kwa macho na kutumia vifaa maalumu (Visual Inspection), 2) matumizi ya vimiminika ili kugundua nyufa ndogo zisizoweza kuonekana kwa macho (Liquid Penetrant Inspection), 3) matumizi ya sumaku na usumaku kutoka kwenye umeme kugundua nyufa ambazo hazionekani kwa macho (mlMagnetic Particle Inspection), 4) matumizi ya mawimbi ya sauti kugundua mapungufu yaliyo ndani ya kitu (Ultrasonic Inspection), na 5) matumizi ya mionzi kigundua mapungufu ya kitu yaliyo ndani (Radiography Inspection).