Home LOCAL TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA KWANZA MWAKA WA MASOMO 2024/25

TCU YAFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI AWAMU YA KWANZA MWAKA WA MASOMO 2024/25

Katibu Mtendaji wa Tume ya vyuo vikuu nchini, Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Julai 15, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2024/2025
Na; Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025 kkuanzia leo Julai 15, 2024 huku ikianisha sifa zinazohitajika kwa wanafunzi kusoma katika vyuo vikuu mbali mbali nchini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 15,2024 kwenye Ofisi za Tume hiyo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji TCU Profesa Charles Kihampa, amesema Dirisha hilo limefunguliwa ili kutoa fursa kwa waombaji wa udahili kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia tovuti ya TCU au tovuti za Vyuo mbalimbli vinavyotoa elimu ya juu, nakwamba dirisha hilo litkuwa wazi hadi Agosti 10 mwaka huu.

‘Waombaji wote wa udahili kwa mwaka wa masomo 2024/2025 wanatakiwa kuwa na sifa stahiki za kidato cha sita, sifa stahiki za Stashahada na Cheti cha awali.
Aidha Prof. Kihampa amewapa tahadhari waombaji wote wa shahada ya kwanza ikiwa watahitaji kupata ufafanuzi wa suala lolote juu ya udahili kuwasiliana moja kwa moja na vyuo vikuu husika ama TCU.
“Tunawaasa wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini” amesema Prof. Kihampa.
Amesema masuala muhimu ambayo waombaji wanapaswa kuzingatia ni pamoja na kusoma kwa makini mwongozo wa udahili uliotolewa na TCU pamoja na maelekezo mahususi ya vyuo kabla ya kuanza kutuma maombi ya udahili.
“Waombaji wenye vyeti vilivyotolewa na mabaraza ya mitihani nje ya nchi wanapaswa kuwasilisha vyeti vyao katika Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ili kuweza kupata ulinganifu na matokeo yao yaweze kupatikana kwenye mfumo’

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here