Home Uncategorized TASAC YAFANIKISHA KUPATIKANA JAHAZI LA MIZIGO LILILOPOTEA KIGOMA

TASAC YAFANIKISHA KUPATIKANA JAHAZI LA MIZIGO LILILOPOTEA KIGOMA

Shirika la uwakala wa meli Tanzania. (TASAC) kupitia. Mkoa wa kigoma imepokea taarifa ya kupotea kwa jahazi la mizigo liitwalo MV AMINA ambalo limesajiliwa na TASAC kwa namba za usajili TKG 002449.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TASAC imeeleza kuwa Shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za kiserikali zmeratibu utafutaji na uokozi pamoja na jeshi la polisi na wanamaji katika kufanikisha upatikanaji wa Jahazi hilo.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa jahazi hilo lenye urefu wa mita 18 lilikuwa na mabaharia nane kutoka nchini Tanzania,  iliondoka kwenye bandari ya Ilagala Tanzania saa 10:00 jioni tarehe 27 2024 huku likitarajiwa kuwasili katika bandari ya kalemine nchini Kongo.

Kutokana na uchunguzi ambao umefanyika imebainika kuwa kumekuwa na changamoto ya mtambo uliopelekea Jahazi hilo kupoteza mwelekeo wa mabaharia waliokuwa kwenye Jahazi hilo mbao walipelekwa kwenye mwalo wa sunuka kigoma.

Katika hatua nyingine TASAC imewaomba wananchi na wadau katika kutoa taarifa kupitia kwenye kituo cha kuratibu na utafutaji na uokoaji (MRCC) pindi dharura zinapotokea majini.

Previous articleWAZIRI MKUU: SERIKALI IMEIMARISHA NGUVUKAZI SEKTA YA AFYA
Next articleZIARA YA Dkt. NCHIMBI  YATIKISA UPINZANI,  YAFYEKA ACT, CUF NA CHADEMA KUSINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here