Home BUSINESS TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA PILI UTALII WA VYAKULA ASILI AFRIKA 

TANZANIA MWENYEJI KONGAMANO LA PILI UTALII WA VYAKULA ASILI AFRIKA 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema Tanzania imepata fursa ya kuwa Mwenyeji wa Kongamano la Pili la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN ),Kanda ya Afrika kuhusu utalii wa vyakula vya asili litakalofanyika mwaka 2025.

Ameyasema hayo leo jijini Victoria Falls nchini Zimbabwe katika Kongamano la kwanza la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UN Tourism ) kuhusu Utalii wa vyakula vya asili katika Bara la Africa.

Amesema ni fursa ya kukuza mnyororo mzima wa thamani katika utalii hasa Utalii wa vyakula na itawagusa wadau wengi wakiwemo wakulima, wafugaji ,wavuvi, wazalishaji wa nafaka,wachakataji mafuta n.k

Ameongeza kuwa Kongamano hilo litaambatana na mashindano mbalimbali kwa ajili ya ubunifu ambapo wenye vyuo na wataalamu wengine watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na wenzao kutoka nchi nyingine za Afrika na duniani kwa ujumla.

Previous articleWAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NDANDA, NACHINGWEA
Next articleSAMIA ASISITIZA UMUHIMU WA UHURU WA HABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here