Treni ya Abiria ya SGR imeanza safari zake kwa mara ya kwanza July 25,2024 kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia aliagiza hadi kufikia mwishoni mwa mwezi July mwaka huu safari hizo ziwe zimeanza.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa ni miongoni mwa waliosafiri na treni hiyo leo ambapo amemshukuru Rais Dkt. Suluhu kwa kuwezesha kukamilika kwa reli na safari hizo kuanza.