Rais wa Tanzania Dk. Suluhu Hassan amesema kuwa mauzo ya nje ya bidhaa za zetu nchini yalipanda kutoka shilingi trilioni 12.3 mwaka 2019 hadi kufikia shilingi trilioni 17.3 sawa na dola za Marekani bilioni 6.56 mwaka jana.
Rais Dk. Samia ameyasema hayo leo Julai 3 jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (DIT) maarufu sabasaba yaliyofunguliwa rasmi na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi
“Tutakamilisha miradi ya miundombinu ili bidhaa zinazozalishwa ziweze kufika kwa urahisi kwenye masoko yaliyokusudiwa,” amesema Rais Samia
Amesema serikali itaendelea kujenga, kuboresha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ili kuhakikisha wanaongeza tija kwa uzalishaji kwa wingi na sifa.
Aidha amesema maonesho hayo ya sabasaba kwa mwaka huu yamezikutanisha zaidi ya kampuni 3486 ya ndani nan je ya nchi na kwamba hiyo inaonesha ukuaji na mvuto wa jambo hilo.
“Mvuto huu umechangiwa na juhudi za serikali katika kusimamia misingi imara na thabiti kwenye kujenga uchumi jumuishi na shindani kiwenye nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, viwanda na uwekezaji.
“Ni ukweli usiopingika njia moja wapo ya kufikia hazma hii ni uendelezaji na uimarishaji wa ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa na hivyo kufungia fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji,” amesema.
Hata hivyo amewataka wafanyabiashara kutumia maenesho hayo kukuza biashara zao na kuzitumia taasisi za serikali kufanikisha azma hiyo ya kufanya biashara kwenye nchi za nje hasa eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA).
“Wafanyabishara kutoka Tanzania kupitia maonesho haya jifunzeni kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ili muweze kukuza biashara zenu, itumieni Tantrade kufanikisha biashara zenu kwa kutazama fursa zilizopo kwenye masoko ya kimataifa,” amesema
Amesema Mwaka 2023 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilisajili miradi 504 yenye thamani ya dola za Marekani Bilioni 5.68 hii ni kwa sababu watu wanakuja Tanzania wanaona maonesho hayo na kuvutiwa kuwekeza.
Akizungumza Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi akifungua maobesho hayo amesema kuwa anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuisaidia nchi yake katika kupambana na suala la ugaidi ambalo amelitaka kuwa lilikuwa linazorotesha uchumi wa nchi hiyo.
Amesema Tanzania imesimama pamoja na watu wa Msumbiji kipindi chote mpaka sasa hali katika nchi hiyo imetulia.
Amesema utulivu na amani ni muhimu kwa matumizi ya fursa za nishati kati ya nchi hizo mbili zenye akiba kubwa ya gesi asilia katika mkoa wa Mtwara na jimbo la Delgabo Msumbiji.
“Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ambayo ni kati ya mwaka 2018 na 2023 jumla ya biashara za nje za nchi hizo mbili katika uagizaji na mauzo ya nje yalifikia dola za Marekani Milioni 250 tu”amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omary Saidi Shabani, amesema maonyesho hayo yamepata bahati ya kuwa na marais wawili, huku akisema washiriki wote ni 3846 wa ndani ni 3433 huku akisema kuwa maonyesho hayo yamejumuisha nchi 26 kulinganisha nchi 19 za mwaka jana zikiwemo za Afrika na Ulaya.
Amesema washiriki hao kutoka nje ya nchi, wamefika kuonyesha Teknolojia mbalimbali, huku akitaka Watanzania kuendelea kushiriki na kujifunza kupitia maonyesho hayo.
“Wizara inaendelea kufanya ukarabati wa barabara za ndani ya maonyesho, kujenga jengo la kisasa la maonyesho, kuandaa mikutano na kuboresha Teknolojia huku akiahidi kuendelea kuboresha maeneo ya biashara,” amesema.
Kwa upande wa masoko, amesema wanaendelea kuweka mkazo katika masoko ikiwemo fursa ya soko huru Afrika, huku akisema kuwa wizara imeendelea kutekeleza mfumo wa dirisha moja ambao utaanza kufanya kazi mwaka huu.
Awali Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amemshukuru Rais Dk.Samia kwa akimkaribisha Rais Nyusi kuwa mgeni rasmi wa maonyesho hayo ya Kimataifa ya 48, kwani inaendelea kudumisha umoja na ushirikiano.
Amesema maonyesho hayo yamekuwa yakikua kila mwaka kutoka na ukubwa wake ambapo kwa mwaka jana walifika washiriki 3500 huku mwaka huu imeongezeka ambapo hadi jana walikuwa wamefika washiriki 3846.
Amesema tukio hilo linaonyesha ambavyo nchi zote mbili zinathamini maendeleo ya biashara ambapo jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika hukul akiwakaribisha wananchi na waonyeshaj kupata maarifa na masoko ya biashara na kuongeza juhudi zaidi.
Amesema wataendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuboresha maonyesho kuhakikisha kuwa maonyesho hayo yanaendelea kukua zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu, viwanda, biashara, kilimo na mifugo , Deudatus Mnyika, alisema kuwa maonyesho hayo ni kipimo cha maboresho makubwa ya sekta ya viwanda na biashara ambapo makampuni 3280 yameshiriki yakiwemo ya ndani ya nje ya nchi.
Kuhusu Kituo cha Uwekezaji wa EACLC kilichopo Ubungo, alisema mradi huo umeshatoa ajira 2500 huku ajira 15,000 ni za moja kwa maja na ajira 50,000 zisizo za moja kwa moja ambapo alimkaribisha Rais Dk.Samia katika ufunguzi wa kituo hicho.
Akitoa salama za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aliwapongeza viongozi kwa kutembea kilometa 13 wa miguu katika maonyesho hayo, jambo ambalo limeonyesha uimara wao na kuleta hamasa zaidi katika maonyesho hayo.
Amesema kuwa, wananchi wa Mkoa huo, wamefarijika sana kwa namna anavyoimarisha diplomasia ya mataifa mbalimbali ikiwemo Msumbiji ikiwa ni njia ya kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi.
Amesema wamejipanga vyema kuhakikisha suala la usalama linakuwepo ulinzi wakutosha kuendelea kuboresha na kuhamasika kushiriki huku akiwa vutia wananchi wengi kushiriki.
Amesema zaidi ya nchi 26 zimeshiriki katika maonyesho hayo ikiwa ni matunda ya kuimarisha kwa deplomasia, huku akimkaribisha Rais Nyusi kupata makazi katika Mkoa huo na kufanya uwekezaji Zanzibar ambako ameandaliwa eneo maalumu.