Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Katavi tarehe 15 Julai 2024 ambapo wananchi wa Mpimbwe waliambiwa kuwa bei ya mahindi itaanzia shilingi 600.
Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa mkoani Katavi kwa siku tatu ambapo pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, alizindua pia vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), na kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka za aina tofauti kutoka tani 5,000 hadi tani 28,000.
Ziara hiyo pia imeshirikisha Viongozi wa Serikali akiwemo Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo.