Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria ununuzi wa nafaka kwa msimu wa 2024-2025 mara baada ya uzinduzi wa vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia Nafaka ya (NFRA), Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi mkoani rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA) Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa
tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Rukwa kilichopo Kata ya Momoka, Sumbawanga tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Adolph Mkenda wakati akimuonesha Majengo ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga yaliyopo Kata ya Momoka tarehe 16 Julai, 2024.
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambacho ambacho kipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana.