Home BUSINESS PURA KUANZA KUTANGAZA MAENEO MAPYA YA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI

PURA KUANZA KUTANGAZA MAENEO MAPYA YA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI

Na: Mwandishi wetu

Katika Kuendelea kutangaza maeneo mapya ya uwekezaji nchini hususani  kwenye vitalu vya Mafuta na Gesi,  Mamlaka. ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), kwa sasa inatarajia kuanza kutangaza maeneo mapya katika Ukanda wa Pwani hivi karibuni kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye Banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Sangweni amesema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kufanya tafiti kwenye baadhi ya maeneo tofauti nchini, na kubainisha kuwa asilimia 50 ya eneo lote nchini lina miamba tabaka yenye mafuta, nakwamba katika maeneo hayo mengi yako Ukanda wa Pwani, Kati na Nyanda za Juu maeneo ya Mbeya.

“Hivi karibuni tunatarajia kuanza kutangaza fursa za uchimbaji Katika Ukanda wa Pwani na kuendelea kwenye baadhi ya maeneo mengine ikiwemo Singida na eneo la Kyela mkoani Mbeya” amesema Mhandisi Sangweni.

Aidha, ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo PURA inaendelea kutoa Elimu kwa wananchi na washiriki wote kuifahamu Mamlaka hiyo na namna inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here