Home LOCAL PROF. MKENDA: MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ANAEFANYA UDANGANYIFU ATAFUKUZWA CHUO

PROF. MKENDA: MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ANAEFANYA UDANGANYIFU ATAFUKUZWA CHUO

Waziri wa Elimu Tayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo Julai 12,2024 kwenye Ofisi za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Jijini Dar es salaam. (Kushoto), ni Karibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa.

DAR ES SALAAM 

Waziri wa Elimu Tayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amewataka wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wakati wa mitihani, nakwamba atakayebainika hatua kali dhidi yake zitachukuliwa ikiwemo kufukuzwa chuo papo hapo.

Waziri Mkenda ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo Julai 12,2024 kwenye Ofisi za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani ya wanafunzi wa Vyuo vikuu na kuripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na kuleta taharuki kwa Jamii.

Amesisitiza kuwa endapo mwanafunzi atabainika kufanya vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani atatimuliwa chuoni mara moja.

Aidha amewataka kuacha kutumia baadhi ya watu wenye vyeo Serikalini kutaka kuwasaidia, nabadala yake wafuate utaratibu wa kisheria.

“Wizara haitoingilia maamuzi ya vyuo vikuu pindi mwanafunzi anapochukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu ikiwemo wanaofanya vitendo vya udanganyifu kwenye mitihani.

“Ni vema wanafunzi wa vyuo vikuu wanapofanya mitihani wapimwe kwa usawa na haki sio kufanya udanganyifu wakati kuna wengine wanatumia juhudi zao na maarifa” amesisitiza Prof. Mkenda.

Previous articleRAIS SAMIA AWASILI KATAVI KWA ZIARA YA KIKAZI
Next articlePURA KUANZA KUTANGAZA MAENEO MAPYA YA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here