Home BUSINESS OREXY GAS YAMTANGAZA SHILOLE KUWA BALOZI WAKE WA UHAMASISHAJI

OREXY GAS YAMTANGAZA SHILOLE KUWA BALOZI WAKE WA UHAMASISHAJI

DAR ES SALAAM 

KAMPUNI ya Gesi ya Oryx imemtangaza Mama Lishe Zuwena Mohamed maarufu Shilole (Shishifood) kuwa balozi wao katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kupikia kupitia mitungi ya gesi nchini.

Lengo la Oryx kumpa Ubalozi Shilole unalenga kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatuminia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza wakati wa tukio hilo lililofanyika Julai 4 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Shaban Fundi amesema wameamua kumchagua Shilole kwasababu ni miongoni mwa wadau wanaohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema kupitia kwa Shilole wanaamini kuna wengine ambao walikuwa nyuma kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kuendelea kutumia gesi za Oryx kupikia.

“Tunafamu Shilole amekuwa mjasiriamali maarufu machi, anamiliki migahawa ya Shishifood katika miji ya Dar es Salaam na Dodoma, amekuwa mama Lishe wa kisasa na muumini mzuri wa kutunza mazingira,hivyo Oryx tunaona fahari kumtangaza Shilole kuwa balozi wetu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kwa pamoja kufikia malengo ya Rais Samia ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.”

Kwa upande wake Shilole ambaye pia ni Msanii maarufu nchini,amesema yupo tayari kushirikiana na wadau wengine kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema Kampuni ya Oryx imekuwa ikiweka jitihada kubwa kuhamasisha matumizi nihati safi ya kupikia kwa Mama lishe na baba lishe nchini, hivyo ameona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa ushirikiano.

Msanii na Mama Lishe Zuwena Mohammed maarufu Shilole akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kuwa Balozi wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia gesi ya Oryx.Kulia ni Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Shaban Fundi na kushoto ni Meneja Miradi ya Nishati safi ya kupikia kutoka katika Kampuni hiyo Peter Ndomba

Msanii maarufu nchini ambaye pia ni Mama Lishe Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ulazima wa kutumia nishati safi ya kupikia.Shishi ametangazwa na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania kuwa Balozi wao kwa ajili ya kushirikiana katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kutumia gesi ya Oryx .Kushoto ni Meneja Miradi ya Nishati safi Oryx Gas Peter Ndomba.

Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi akimueleza jambo Mama Lishe na Msanii wa Bongo Fleva Zuwena Mohammed maarufu Shilole baada ya Kampuni hiyo kumtangaza kuwa Balozi wao ambaye atakuwa akihamasisha nishati safi ya kupikia NCHINI 

Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya kumtangaza Mama Lishe na Msanii Zuwena Mohammed maarufu Shilole (katikati) kuwa Balozi wao ambaye atakuwa akihamasisha nishati safi ya kupikia.Kushoto ni Meneja Miradi ya Nishati safi Oryx Gas Peter Ndomba.

Previous articleRIBA YA BENKI KUU YASALIA ASILIMIA 6
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO JULAI 5-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here