Home BUSINESS NI MUHIMU WAHANDISI WA NIRC KUSAJILIWA ILI KUENDANA NA KASI YA UWEKEZAJI...

NI MUHIMU WAHANDISI WA NIRC KUSAJILIWA ILI KUENDANA NA KASI YA UWEKEZAJI WA RAIS SAMIA – MNDOLWA

NiRC Dodoma

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imesema kutokana na uwekezaji mkubwa alioufanya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya umwagiliaji ni muhimu wahandisi wa taasisi hiyo kusajiliwa.

Lengo ni kuhakikisha wanaosimamia miradi hiyo wanakidhi vigezo na wanatambua wajibu walionaona kwa Taifa na kuacha kuwabeba wakandarasi wasiofaa.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) Bw. Raymond Mndolwa.

Aidha akimkaribisha Mrajisi kutoka Bodi ya Usajili Wahandisi nchini, bwana Bernard Kavishe, katika mafunzo ya kuwajengea uelewa wahandisi wa Umwagiliaji kutoka mikoa yote nchini, wanaohudhuria mafunzo ya Mfumo Mpya wa Usimamizi wa Makusanyo Ada ya Umwagiliaji,iMIS,Mndolwa amehimiza kuwa ofisi yake itaendelea kuwaunga mkono wahandisi ambao wapo tayari kujisajili ili kutimiza takwa hilo la
kisheria

Amesisitiza kuwa, tangu Uhuru wa nchi, serikali ya Rais Dk. Samia imetoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji hivyo wahandisi wawe sehemu ya kuweka alama ya kusimamia kazi hizo ipasavyo.

Bw. Mndolwa, amewahimiza wahandisi wanaofanya kazi NIRC wahakikishe wanakidhi vigezo vinavyohitajika kihandisi, kwa mujibu wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi nchini, ili kuweza kufanya kazi zenye ubora na viwango.

“Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya jambo la kihistoria kuwekeza fedha nyingi zaidi ya Bilioni 400, haijawahi kutokea tangu Uhuru wa nchi hii katika kilimo cha Umwagiliaji hapa nchini. Wahandisi mnao wajibu mkubwa kuhakikisha mnasimamia miradi ya ujenzi kwa weledi na uzalendo ili kuhakikisha uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na serikali unakwenda kuwanufaisha wakulima na kuleta maendeleo endelevu,”alisema.

Mndolwa pia amewahimiza wahandisi wa NIRC kutumia fursa iliyopo, kuchota maarifa na ujuzi kutoka kwa wakandarasi wa kigeni, kwa lengo la kujiimarisha katika utendaji.

Kwa upande wake, Mhandisi Kavishe amewataka wahandisi hao wa Tume kuzingatia sheria na vigezo vya taaluma hiyo hususani katika kusajiliwa.

“Bodi ya Usajili Wahandisi inawajibu wa kuhimiza wahandisi wote na Wataalam Washauri wa ndani na wanaotoka nje ya nchi, kuhakikisha wanasajiliwa na kutambuliwa na bodi na NIRC mkiwa taasisi ya umma msimamie hilo, wenzetu madaktari hawezi kufanya kazi ya upasuaji bila kusajiliwa nasisi tuna wajibu wa kusajisajili ili miradi hii iweze kuwa salama,”alisema.

Amesisitiza kuwa, wahandisi wa NIRC wanacho cha kujivunia kwa uwezeshaji wa usajili wanaofanyiwa na uongozi wa Tume na ni vyema kutumia nafasi hiyo ipasavyo.

Akihitimisha,Mndolwa amesisitiza wahandisi wa umwagiliaji na watumishi wengine wa tume, kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuheshimu sheria za nchi na mamlaka za serikali, kwa lengo la kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wakulima na wadau wengine wa umwagiliaji hapa nchini , na kwamba kufanya hivyo kutasaidia kuhakikisha kuwa miundo mbinu inayojengwa inakuwa bora na ya kudumu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadae.

 

Previous articleTUMIENI FAFITI ZA CBE KUKUZA BIASHARA NCHINI – DKT. ABDALLAH
Next articleRAIS SAMIA NA RAIS FILIPE NYUSI WA JAMHURI YA MSUMBIJI WATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA 48, SABASABA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here