Home LOCAL NI KISHINDO CHA BALOZI NCHIMBI ZIARANI MTWARA

NI KISHINDO CHA BALOZI NCHIMBI ZIARANI MTWARA

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akiambatana na Wajumbe wa Sektarieti ameendelea na Ziara yake Mikoa Miwili ya kusini ambayo ni Lindi na Mtwara leo tarehe 29 Julai 2024 amesalimia na kuzungumza na Wananchi wa Jimbo la Mtwara Vijijini Kata ya Mpapura ambalo liko Upinzani

Balozi Nchimbi amesema pamoja na kwamba Jimbo hili liko Upinzani lakini Utekelezaji wa Ilani hapa ni wakiwango cha Juu kwani tumeweka Kaimu Mbunge Mhe Chikota anaefanya shughuli hapa hakika kazi Imefanyika nafikiri mmeona sasa kazi kwenu wakati ukifika ibidi mbadilike kwani mnapata Maendeleo lakini hamna wa kumhoji pamoja na yote CCM inawafanyia mambo makubwa tumeyasikia hapa wenyewe sasa wakati ukifika pigeni chini wasiobadilika kichagueni Chama cha Mapinduzi.

Mwisho akawaasa Wananchi kuendelea kutunza na kulinda asitokee Mtu akawadanganya watu kuhusu kuharibu amani yetu amani tuliyonayo huku akichangia Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kumalizia Ujenzi wa Ofisi ya Chama Wilaya Mtwara Vijijini.

29 Julai,2024. Siku ya pili

#VitendoVinasauti
#TunaendeleanaMama
#Kaziiendelee

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here