* mamia ya wanachama wajiunga CCM*
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi leo Jumatano, 31 Julai 2024, akiwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mchinga, kwa ajili ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo, Mama Salma Rashid Kikwete, amepokea mamia ya wanachama wa vyama vya upinzani, wakiongozwa na waliokuwa madiwani pekee wa Vyama vya CUF na ACT jimboni hapo.
Balozi Nchimbi amepokea mamia ya wanachama na viongozi hao, wakiwemo Mhe. Hussein Kimbyoko aliyekuwa Diwani wa Kata ya Milola (CUF) na Mhe. Athumani Maije aliyekuwa Diwani wa Kata ya Rutamba (ACT), siku moja tu baada ya kuwapokea viongozi waandamizi wa vyama hivyo, pamoja na Chadema katika Mkoa wa Lindi, waliohama wakiwa na mamia ya wanachama wa vyama hivyo vya upinzani na kujiunga CCM.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi ya Chama cha ACT, Ndugu Rutamba, amesema:
“Nitakuwa mnafiki kweli kwa mambo makubwa yaliyofanyika Jimbo la Mchinga, naona aibu kuendelea kubakia kupinga kila kitu wakati kazi kubwa ya maendeleo inafanyika…ilani nimetekeleza wakati sio yangu, napokea posho ya Serikali ya CCM na kazi kubwa anayoifanya mbunge wangu Mama Salma Kikwete nimeona nibwage manyanga ya ACT Wazalendo nakuhamia CCM naomba ushirikiano kwenu tuchape kazi.”
Nae Ndugu Hussein Kimbyoko amesema “Wanamchinga kama mlivyosikia ni maamuzi magumu mtu kuacha kazi yake lakini nimekaa nimetafakari kwa kazi kubwa aliyoifanya Dkt Samia Suluhu Hassan nimeona nimuunge mkono kwa kujiunga CCM. Pia Mbunge pamoja na kwamba sikuwa CCM lakini alikuwa akinishirikisha kwa kila jambo sasa nami ni CCM naomba ushirikiano wenu kwani mimi mmesajili mtu kweli kweli.”
Balozi Nchimbi amewakabirisha CCM mamia ya wanachama hao wapya kutoka vyama vya upinzani.
“Tunawashukuru sana madiwani wote wawili waliokuwa upinzani kurudi CCM na wanachama wengi tuliopata leo. Wamekiri wenyewe vizuri hapa kuwa hii ni kutokana utekelezaji mzuri wa ilani kwenye jimbo na kazi bora zilizofanywa na Rais na Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia Suluhu Hassan naomba sasa tushirikiane kuzidi kukiimarisha CCM na kuendelea kujenga nchi yetu,” amesema Balozi Nchimbi.
31 Julai, 2024, Lindi Vijijini Jimbo la Mchinga