Home BUSINESS NAIBU KATIBU MKUU- WIZARA YA FEDHA ATEMBELEA BANDA LA BOT MAONESHO YA...

NAIBU KATIBU MKUU- WIZARA YA FEDHA ATEMBELEA BANDA LA BOT MAONESHO YA SABASABA

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo  (kulia), wakati wa ziara ya Naibu Katibu huyo, kutembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) , yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Myerere Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo  (kushoto), akizungumza na maafisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alipotembelea Banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Myerere Jijini Dar es Salaam, (Kutoka kulia), ni Vivian Kezara, Sabitina Haji, na Gloria Chellunga, maafisa kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha Benki Kuu ya Tanzania.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo  (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, BOT,  Bw. Deogratias Mnyamani, (kushoto), wakati Kiongozi huyo alipofanya ziara kutembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Sabasaba, Dar es Salaam

Meneja Uendeshaji Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bw. Nkanwa Magina. (wapili kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo (Kulia)  kuhusiana na huduma wanazozitoa kwenye kurugenzi yao. (wakwanza kushoto), ni Bw. Denis Mrema na (wa tatu kushoto), ni Bi. Thuwaiba Juma maafisa kutoka DIB.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo  (wakwanza kulia), akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Maafisa Kutoka kurugenzi Bodi ya Bima ya Amana (DIB), mara baada ya kusikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja  wa Bodi hiyo, Bw. Nkanwa Magina. (wapili kulia), ni Gavana wa BoT Bw. Emmanuel Tutuba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo (kushoto),  akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha, Bw. Emmanuel Akaro. (watatu kulia), mara baada ya Naibu Katibu Mkuu kufika kwenye kurugenzi hiyo kufahamu namna wanavyotekeleza majukumu yao. (Kutoka kulia) ni maafisa kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Bw. Joshua Mganga, Bw. Mussa Ambika na Bw. Enthusiasm Mwagala.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kushoto), akimkabidhi zawadi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bi. Jenifa Christian Omolo  (kulia), mara baada ya Kiongozi huyo kutembelea Banda la BoT kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Previous articleOSHA YAPIMA WANANCHI 300 SABASABA 
Next articleJAFO AHIMIZA SEKTA YA VIWANDA KUUNGWA MKONO KUFANIKISHA JITIHADA ZA RAIS KATIKA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here