KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Felician Mramba, amesema Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha udhibiti wa bei ya bidhaa, unaimarika mara dufu ili wananchi wazidi kunufaika na uwekezaji unaofanywa na Serikali yao pendwa, inayoongozwa na Mhe. Ris Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameyasema hayo Julai 9, 2024, alipotembelea Banda la EWURA katika Maoneshoa ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa udhibiti wa bei ya bidhaa, nchini umeimarika ukilinganisha na nchi nyingine, nakwamba Tanzania ni nchi yenye bei ya nchini za nishati ya umeme.
“Nchi yetu ni yenye bei ya chini ya umeme, hata ukilinganisha na nchi majirani zetu utabaini hili.
“Kadhalika aupatikanaji wa huduma hii umeimarika sana, hatusemi kwamba ubora umetulia mahali ambapo hamna shida, hapana ila angalau tupo kwenye ubora mzuri,” amesema Mramba.
Kuhusu Gesi asilia amesema wanafanya vizuri kutoa leseni kwa wale wanaotaka kuchimba visima ili jamii inufaike.
Amesema serikali inaendelea kuisimamia vyema mamlaka hiyo ili itekeleze vyema majukumu yake.
Amesema pia zipo huduma za kiushauri na malalamiko ambazo EWURA wanatoa kwa wananchi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa EWURA, Dkt. James Andilile ameahidi kuwa wataendelea kuhakikisha huduma wanazotoa za umeme na gesi asilia zinaendelea kupatikana katika ubora unaotakiwa.
Amesema pia kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya uwekezaji na mwezi uliopita walitiana saini ya kupimana utendaji kazi.
Amesema pia wanatekeleza majukumu mbalimbali ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya umeme hususani Mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa upande wa sekta ya mafuta, amesema wanaendelea kufuatilia ubora wa mafuta na hadi Juni 30 habari ya ubora wa mafuta ulikuwa umefikia asilimia 97.
Amesema lengo ni kuhakikisha mafuta yanauzwa kwenye ubora unaotakiwa na kufuatilia mwenendo wa bei za soko la dunia ili kuangalia unafuu wa bei kwa wananchi.
Ameahidi kuendelea kutoa bei za kila mwezi na kwamba wamegeukia pia gesi ya kwenye magari na kuwapo kwake kumesaidia kupunguza matumizi ya Dola nchini kwasababu huduma hiyo inapatikana Tanzania.
Kuhusu sekta ya maji amesema wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa huduma na kila eneo serikali inafanya uwekezaji ambao utasaid.