Home BUSINESS MKURUGENZI WA TIC AELEZA FAIDA ZA UBORESHWAJI WA SHERIA YA UWEKEZAJI

MKURUGENZI WA TIC AELEZA FAIDA ZA UBORESHWAJI WA SHERIA YA UWEKEZAJI

Dar es Salaam.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri amesema kuwa kuboreshwa kwa sheria mpya ya uwekezaji imeibua faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha mtaji kutoka Dola za Marekani 100.000 mpaka 50.000 kwa Watanzania ili kuwawezesha kuwekeza kwa urahisi zaidi.

Teri ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa wawekezaji Wazawa waliosajili miradi yao Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), uliofanyika leo Julai 25,2025 Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa mkutano huko umelenga kujadili maboresho ya  sheria ya Uwekezaji namba 10 ya mwaka 2022, sura namba 38 ambayo imeikasimisha TIC jukumu la kuratibu, kuhimiza, kuhamasisha, na kuwezesha uwekezaji Tanzania, sambamba na kuishauri Serikali kuhusu sera ya uwekezaji na mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji nchini.

kuna vivutio vipya ambavyo vimewekwa kwa Watanzania ambao tayari wameshawekeza lakini wanataka kukuza uwekezaji wao, na kuboresha wawekezaji wapya.

“Tunaweza kukupatia vivutio vya uwekezaji sio tu pale unapoanza bali pia pale ambapo unaendeleza na kukuza uwekezaji wako” ameeleza.

Ameongeza kuwa mkutano huo ni fursa kwa wawekezaji hao kupata majibu kutoka kwa Taasisi zilizopo kwenye kituo cha pamoja (one stop center), ambazo ni pamoja na BRELA, NEMC, TRA, Uhamiaji, Idara ya Kazi, NIDA ambapo zitahusika katika mchakato wa uwekezaji.

Amekisisitiza umuhimu wa uwekezaji wa ndani ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa nakubainisha kuwa TIC imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na kuwahakikisha huduma bora zinazohitajika ili kuendesha miradi yao kwa ufanisi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here