Home LOCAL MKURUGENZI MKUU MSD: TAASISI YETU IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA KIUTENDAJI

MKURUGENZI MKUU MSD: TAASISI YETU IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA KIUTENDAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari baada ya kufanya ziara ya kutembelea ghala la kuhifadhia bidhaa za afya Dodoma pamoja na ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia bidhaa hizo mkoani Dodoma.

Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (kulia) akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari walipofanya ziara ziara ya kutembelea ghala la kuhifadhia bidhaa za afya  pamoja na ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia bidhaa hizo mkoani Dodoma.

Na: MWANDISHI WETU – DODOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai, amesema kuwa taasisi yake imepata mafanikio makubwa ya kiutendaji na kuimarisha huduma zake kwa kufanya ununuzi na usambazaji wa vifaa tiba vinavyohitajika katika vituo vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi vituo vinavyotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini ili kufanikisha upatikanaji wa huduma Bora kwa wananchi.

Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini Julai 3,2024 Jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na mtaji wa kiasi cha fedha Shilingi bilioni 100 kilichotolewa na Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kuiwezesha MSD kuendelea kukabiliana na changamoto za mnyororo wa ugavi na kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini

Aidha ameongeza kuwa kutokana na maboresho yanayoendelea kufanya na Serikali, mapato ya MSD yameendelea kuongezeka Kutoka Shilingi billioni 359.6 kwa mwaka wa fedha 2023/24, ikiwa ni ongezeko la Shilingi bilioni 150.43 sawa na asilimia 42.

“Fedha hizi zimesaidia MSD kuwa na uwezo wa kuhudumia mahitaji ya vituo kwa wakati na kutengeneza mikakati ya itakayofanya Taasisi iendelee kununua kwa tija na kuimarisha mahusiano na wazabuni mbalimbali. Mafanikio mengine ni kuimarika kwa makusasanyo ya Fedha kutoka vituo vya kutolea huduma za afya,” amesema Tukai.

Amefafanua kuwa mwaka 2024 umekuwa wa manufaa makubwa kutokana na mpango kazi na mikakati waliyojiwekea inatekelezeka kwa kasi kubwa na kwa vitendo.

Awali Wahariri wa Vyombo vya Habari walipata fursa ya kujionea namna MSD inafyofanya shughuli zake kwa kutembelea ghala la kuhifadhia Dawa linanalohudumia mikoa ya Kanda ya Dodoma , Singida na Tabora, na kujionea mradi wa ujenzi wa ghala kubwa na la kisasa ambalo ujenzi wake upo umefikia asilimia 60 na unatajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here