Home LOCAL MELI YA MATIBABU ISIISHIE DAR PEKEE

MELI YA MATIBABU ISIISHIE DAR PEKEE

Na – WAF – Dar Es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameliomba Jeshi la Ukombozi la watu wa China lililowasili nchini kwa huduma za Matibabu kupitia Meli yao kutembelea katika Mikoa mingine ya Pwani ya Tanzania ikiwemo Tanga, Lindi na Mtwara pamoja Zanzibar kwa ajili ya kutoa huduma hizo za matibabu pamoja na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu.

Waziri Ummy ametoa ombi hilo leo Julai 19, 2024 katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar Es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana juu ya kuendeleza ushirikiano baina ya Nchi hizo Mbili katika upande wa Sekta ya Afya.

Kwa upande wake, kiongozi wa msafara kutoka katika Meli hiyo ya China Rear Admiral Bw. Ying Hong Bo. amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya ili kudumisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo Mbili.

Meli hiyo iliwasili Nchini Tanzania katika kusheherekea miaka 60 ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na China ambao imekuwa ikitoa huduma za upimaji wa Afya na matibabu kwa Watanzania na wachina wanaoishi nchini tangu tarehe 16/07/2024 hadi tarehe 23/07/2024.

Mhe. Ummy amekutana na Viongozi hao (PLA) wakiongozwa na ‘Rear Admiral’ Bw. Ying Hong Bo ambae ni Mkuu wa Meli ya kivita ya majini ambayo ni Hospitali ijulikanayo kama ‘Ark Peace Hospital’

       

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here