Home BUSINESS JIJI LA MBEYA NA MUWEKEZAJI KUTOKA INDIA WAKUTANA KUJADILI UZALISHAJI WA MBOLEA...

JIJI LA MBEYA NA MUWEKEZAJI KUTOKA INDIA WAKUTANA KUJADILI UZALISHAJI WA MBOLEA DAMPO LA NSALAGA.

Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo tarehe 3 Julai, 2024 imekutana na wawekezaji kutoka Kampuni binafsi ya BA Prerna CleanEarth kujadili uwezekano wa kuwekeza katika dampo la Nsalaga na kuzalisha mbolea inayotokana na taka ninazooza.

Mwakilishi wa Kampuni hiyo kutoka Gujarat India Bw. Parish Kalathia, amesema endapo Jiji litaridhia, kampuni hiyo itachakata taka hizo kwa kutenganisha taka ngumu na zile zinazooza na kisha kuzalisha mbolea zinatotumika mashambani.

Amesema mbolea inayotokana na taka zinazochakatwa haitakuwa na madhara yoyote kwenye ardhi na mimea itakayozalishwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji Bw. John Nchimbi amemshukuru Rais wa Mabunge Duniani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa jitihada anazozifanya za kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza mkoani Mbeya. Jiji limepokea ombi hilo la ushirikiano na kueleza kuwa suala hilo litafikishwa ngazi za juu na endapo itaridhiwa taratibu nyingine zitafuata ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba wa mashirikiano.

Bw. Nchimbi amesema uwekezaji kama huu umefanyika Kilimanjaro na Dar es Salaam na kuleta mafanikio.

“Uwekezaji huu mbali ya kuwa chanzo cha mapato endapo utaridhiwa pia utawanufaisha wakulima kwa kupata mbolea bora na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao mbalimbali,” amefafanua Bw. Nchimbi.

Previous articleRAIS FILIPE NYUSI WA JAMHURI YA MSUMBIJI AFUNGUA RASMI MAONESHO YA 48 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA
Next articleRAIS SAMIA: MAUZO YA BIDHAA NJE YAMEPANDA KUTOKA SH. TRIL. 13.3 HADI KUFIKIA TRIL 17.3
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here