Home LOCAL JET YAWANOA WAHARIRI WA HABARI UHIFADHI NA MAZINGIRA

JET YAWANOA WAHARIRI WA HABARI UHIFADHI NA MAZINGIRA

Mwenyekiti Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Dkt. Ellen Ottaru, akizungumza katika mafunzo kwa wahariri wa habari, yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, yanayofanyika Bagamoyo, Pwani.

Meneja wa ushiriki wa Sekta Binafsi, Mredi wa USAID Tuhifadhi Mazingira, Dkt. Elikana Kalumanga, akitoa wasilisho katika katika Mafunzo kwa Wahariri wa habari, yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, yanayofnyika Bagamoyo Pwani.

Mkurugenzi wa Tanzania Media Fund TMF, Dastan Kamanzi akikitoa mada katika mafunzo hayo.

Mjumbe wa Kamati ya Uendaji, Jukwaa la wahariri Tanzania, TEF, akizungumza wakati wa maswali na kuchangia mada katika mafunzo hayo.

PICHA NA; HUGHES DUGILO

Na Hughes Dugilo, BAGAMOYO.

Chama Cha Wandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kimewapiga msasa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini juu ya umuhimu wa uhifadhi na mazingira.

Mafunzo hayo pia yalikuwa na lengo la kuwapa uelewa Wahariri katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na umhimu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika shughuli za uhifadhi.

Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga amesema kuwa kama sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu inaweza kuendelea kuwa na mchango mkubwa zaidi katika pato la Taifa.

”Ipo haja ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye shoroba za wanyamapori.

“Shughuli za kibimadamu zimekuwa zikifanyika kwenye shoroba hivyo tunahitaji ushiriki wa pamoja katika kulinda na kuhifadhi viumbe hai nchini,” amesema Dk. Kalumanga.

Ameeleza kuwa katika uhifadhi zipo fursa nyingi ambazo Watanzania wakizitumia vizuri hasa katika sekta ya utalii ni fursa kubwa kwao kujiongezea kipato.

“Katika kazi hizi za uhifadhi zipo fursa nyingi,mojawapo ni ya kutumia utalii ambapo uwekezaji wake ni rahisi, ambapo unaweza kuweka matenti na vyoo vya kuhamisha, na watalii wakafurahia na kupata fedha “alisema Dk. Kalumanga.

Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa jamii hasa zile zilizopo katika maeneo yenye kupakana na hifafhi kuzipata fursa hizo ikiwemo kufanya kilimo cha viungo na mbogamboga ambacho hustawi zaidi katika maeneo ya hifadhi.

Dk. Kalumanga alibainisha kuwa kilimo cha viungo na mbogamboga ni biashara yenye tija na faida kwa jamii kwani hata katika mradi huo umekuwa ukisaidia jamii kujiendeleza katika kilimo hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JET, Dkt. Ellen Otaru akifungua semina hiyo, amesema lengo la kukutana na Wahariri ni kupanua wigo wa ufahamu kuhusu uandishi wa taarifa za uhifadhi na mazingira ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Previous articleRAIS SAMIA AWASALIMIA WANANCHI WA KAENGESA MKOANI RUKWA
Next articleKIKAO CHA WADAU WA UMWAGILIAJI MWAMKULU CHAFANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here