Home BUSINESS EWURA YAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA

EWURA YAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA

DAR ES SALAAM 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekusudia kutumia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) katika kutoa elimu kwa wananchi na kuhamasisha kuhusu matumizi ya Nishati safi ya Kupikia.

Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano na Uhusiano EWURA, Titus Kaguo alipozungumza na waandishi wa Habar Julai 5, 2024, kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Myerere Jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kiwa hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Rais Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa na mkakati wa Kitaifa unaolenga kuhakikisha Watanzania wanahamia kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika hatua nyingine Kaguo amesema serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto ikiwemo magari ili kuendeleza matumizi ya nishati safi huku wito ukitolewa kwa wawekezaji kujikita katika uwekezaji wa vituo vya gesi hiyo –CNG.

Pia ameongeza kuwa wanaendelea kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye vituo vya ujazaji gesi asilia na kwamba utaratibu umeweka na TBS kwa kuwezesha kituo cha mafuta kuuza gesi asili kwenye magari” ameongeza Kaguo.

Maonesho ya Sabasaba mwaka huu yamekuwa ni fursa kwa BRELA kukutana na wadau pamoja na wananchi na kutoa elimu kuhusu masuala ya petroli, umeme, gesi, asilia pamoja na maji na usafi wa mazingira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here