Home BUSINESS BODI YA WAKURUGENZI TASAC YAFANYA ZIARA BANDARI YA NYAMISATI PWANI

BODI YA WAKURUGENZI TASAC YAFANYA ZIARA BANDARI YA NYAMISATI PWANI

Na John Bukuku

Bandari ya Nyamisati iliyopo Kibiti mkoani Pwani imetajwa kuwa ni bandari ndogo inayofanya vizuri pamoja na changamoto zinazoikabili ikiwemo ukosefu wa afisa forodha bandarini hapo na mashine ya kunyanyulia mizigo (Fork Lift) hivyo kusababisha ukusefu wa mapato katika bandari hiyo.

Meneja wa Bandari ya Nyamisati Issa Unemba akitoa taarifa kwa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Uwakala Meli Tanzania_ TASAC wakati walipofanya ziara katika bandari hiyo na imekagua uboreshaji wa miundombinu ambayo ya maelekezo waliyotoa kwenye ziara kama hiyo mwaka 2022, amesema kutokuwepo kwa Afisa Forodha huyo ambaye angesimamia ukusanyaji wa mapato kwa mizigo ya kwenda Comoro kunachangia kiwango kikubwa cha upotevu wa mapato.Aidha kutokana na uwepo wa abiria wengi wanaopitia hapo pamoja na mizigo bandari ikiboresha itainua mapato yake zaidi

Ameongeza kuwa bandari ya Nyamisati inasfirisha abiria zaidi 4000 pamoja na mizigo wanaopitia hapa kwenda katika visiwa na maeneo mbalimbali kama vile Mafia, Saninga Karachu, Nchinga na kwingineko kwa hiyo afisa forodha angekuwepo angefanya kazi ya kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuwavuta wateja wa nchi ya Commoro na kuleta tija katika utendaji wa bandari

Amesema kwamba uboreshaji wa miundombinu katika bandari hyo utakapokamilika itasaidia kuongezeka kwa mapato ambapo kwa sasa uboreshaji wake umefikia asilimia 95 k wa maelekezo ambayo bodi hiyo.iliyatoa

Amesema bandari ya Nyamisati ni ya kimkakati katika kuhudumia visiwa vya bahari ya Hindi.Hivyo wamefanya maboresho mengi bandari hapo na wataendelea kuboresha zaidi kwa kuwa vifaa vya kupakia na kupakua mizigo.

“Kama mnavyoona mabadiliko mengi yamefanyika.Bandari yetu inangaa katika kuwahudumia wananchi.Maelekezo ya bodi tumeyatekeleza na tunashukuru sana, tunafarijika kwa ujio wenu tena”, amesema Bw..Issa Unemba.

Ameongeza kuwa bandari ya Nyamisati inatoa huduma kwa zaidi ya visiwa 16 kwa kupeleka mizigo ya vyakula, mavazi,vifaa vya ujenzi na mengineyo.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi bandari hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)Nahodha. Mussa Mandia imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kutekeleza vema maelekezo ya kudhibiti usalama wa abiria na mizigo bandari ya Nyamisati.

“TPA hongera sana kwa kutekeleza maelekezo yetu ya Mwaka 2022 tulipofanya ziara hapa na kuelekeza TPA kuweka utaratibu mzuri wa abiria kuingia kwenye meli, kujenga jengo la kutunzia mizigo na kutenganisha mizigo ya vyakula na mizigo mengine.Yote yametekelezwa na mengine yanaendea kutekelezwa. Hakika tumefurahi kuona maboresho hayo”, amesema Nah.Mandia.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw.Mohamed Salum amesema bandari hii ni mojawapo ya bandari ndogo zinazofanya vizuri katika kutoa huduma ya usafiri.

“Kwa ujumla maelekezo ya bodi yametekelezwa na imetuelekeza tuendelee kusimamia uboreshaji wa eneo la bandari lenye udongo na linaloliwa maji kwa kuwekwa tabaka gumu ili maji yasiendelee kuondoa udongo.Nasisi tutalisimamia hilo.”
Bwana.Salum ameongeza kuwa katika kuweka hali usalama wa uhakika wamejipanga kwa mwaka wa fedha 2024/25 kununua boti 6 za uokoaji na kuzisambaza katika maziwa yetu na ukanda bahari.Navyo vitasaidia kuokoa maisha ya wananchi wanaotumia usafiri majini.

Previous articleWAZIRI KAIRUKI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA PILI WA SHIRIKA LA UTALII DUNIANI NCHINI ZAMBIA
Next articleDIWANI KIMWANGA AFANYA KIKAO NA WAZAZI HOFU UTEKAJI WATOTO 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here