Home BUSINESS BASHE ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA MBEGU ZA MICHIKICHI TARI KIGOMA

BASHE ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA MBEGU ZA MICHIKICHI TARI KIGOMA

KGOMA 

Waziri wa Kilimo m, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ametembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika eneo la Kihinga, Mkoa wa Kigoma tarehe 21 Julai 2024 akiambata na Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana na kukagua shughuli za utafiti wa mbegu za michikichi.

Waziri Bashe alipata wasilisho la hatua za uchavushaji hadi kupata mbegu halisi na bora kwa kutumia tafiti ambazo Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA) hutumia.

Aidha, Waziri Bashe alikagua ujenzi wa jengo la ofisi na maabara ya TARI -Kihinga na kutoa maelekezo ya ukamilishwaji wa ofisi hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya Watumishi na uhalisia wa kuokoa gharama zao za usafiri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here