Home BUSINESS WIZARA YA NISHATI YASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA NISHATI JADIDIFU

WIZARA YA NISHATI YASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA NISHATI JADIDIFU

Akifungua kongamano hilo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC) jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amesema Serikali inajiandaa kuzindua Mkakati na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu ili kuchochea uwekezaji mkubwa katika Nishati Jadidifu.
1000182911

Amesema uzinduzi wa mkakati huo utaakisi vyema Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2015 na makubaliano mengine ya kimataifa na kitaifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

“Kwa kuhama kutoka kwenye matumizi ya mimea asilia kama vile kuni na mkaa wa kupikia, hatupunguzi hewa chafu tu bali pia tunaboresha hali ya hewa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu, utekelezaji wa mkakati huu unasaidia moja kwa moja suala la nishati safi ya kupikia.” Amesema Mha.Luoga
Amesema Serikali pia inaandaa “Mkakati na Mpango Kazi wa Ufanisi wa Nishati Tanzania” utakaosaidia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Nishati na malengo ya kimkakati ya kupunguza kasi ya nishati chafu kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2025 huku lengo la jumla likiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za gharama nafuu na za uhakika za nishati endelevu na ya kisasa kwa wote.
1000182907
Mha. Inocent Luoga aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliowezesha Wiki hiyo kufanyika ikiwemo kampuni ya Sunking, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP); TANESCO, Ensol Tanzania Limited, Global Off- Grid Lighting Association (GOGLA); Africa Enterprise Challenge Fund (AECF) na Umoja wa Ulaya (EU).
Naye Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA) Mha. Mathew Matimbwi, ameiomba Wizara ya Nishati kuwa mwakilishi kutoka sekta binafsi awepo kwenye Bodi ya REA ili kuimarisha utekelezaji wa masuala mbalimbali kuhusu nishati jadidifu.
Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni “Nishati Mbadala kwa Uchumi Shirikishi na Kijani,’
1000182856
1000182859
1000182903
Previous articleWANANCHI WA BUKOMBE WAPEWA SOMO KUHUSU ELIMU
Next articleSTAMICO KUANZA KUUZA MKAA MBADALA KWA JESHI LA MAGEREZA STAMICO (RAFIKI BRIQUETTES)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here