Home LOCAL WAZIRI UMMY AZINDUA KAMPUNI TANZU YA MSD, KUSIMAMIA UZALISHAJI BIDHAA ZA AFYA

WAZIRI UMMY AZINDUA KAMPUNI TANZU YA MSD, KUSIMAMIA UZALISHAJI BIDHAA ZA AFYA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezindua Kampuni Tanzu ya Bohari ya Dawa inayoitwa MSD MEDIPHAM MANUFACTURING CO. Ltd., itakayosimamia viwanda vya kuzalisha bidhaa za afya, pamoja na kuzindua Bodi ya Usimamizi wa kampuni Tanzu hiyo.

Waziri Mwalimu amesisitiza kampuni tanzu hiyo kushirikisha wabia watakaokuwa tayari kushirikiana na MEDIPHAM kuzalisha bidhaa za afya, na kuendelea kutoa kipaumbele wazalishaji wa ndani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Rosemary Silaa ameeleza kuwa kampuni tanzu hiyo ni matokeo ya sheria ya MSD kufanyiwa makekebisho mwaka 2021, na kuongezewa jukumu la kuzalisha bidhaa za afya, hivyo amewaelekeza wajumbe hao wa bodi kuandaa mpango mkakati wa kampuni tanzu hiyo, pamoja na mfumo wa kutathimini namna ya kufikia malengo watakayojiwekea.

Silaa ameeleza kuwa ana imani kuwa kampuni Tanzu hiyo itafanikiwa, ikiwa na mikakati mizuri,akitolea mfano kuwa kiwanda cha barakoa kilianza mwaka 2021 na mtaji wa shilingi Bilioni 1.6 na hadi sasa wameshapata faida ya shilingi Bilioni 4.8.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa tayari kuna viwanda vitatu vinavyozalisha,ambavyo ni pamoja na viwanda viwili vya barakoa (surgical& N95)vilivyopo Keko na kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idofi, Makambako.

Ameongeza kuwa viwanda vingine vilovyopo mbioni kuanzishwa,ni pamoja na kiwanda cha dawa Zegereni Kibaha na kiwanda cha bidhaa za pamba mkoani Simiyu.

Tukai, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya usimamizi wa Kampuni Tanzu (MSD MEDIPHAM) ameeleza kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa inaendelezwa na uendeshaji wake kuwa wenye tija.

Previous articleMBUNGE LUGANGIRA AONGOZA MAANDAMANO KUPINGA UKATILI
Next articleMAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, VIONGOZI WATEMBELEA BANDA LA MSD DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here