Home LOCAL WAZIRI MKUU AZINDUA VITABU VYA HISTORIA YA BUNGE

WAZIRI MKUU AZINDUA VITABU VYA HISTORIA YA BUNGE

DODOMA 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua vitabu vya historia ya Bunge ambavyo vitasaidia kuhamasisha tafiti na kujua zaidi kuhusu mchango wa Bunge katika maendeleo ya jamii nchini.

Amesema kuwa vitabu hivyo pia vitakuwa kielelezo cha mafanikio na changamoto ilizopitia Bunge la Tanzania katika kudumisha demokrasia na utawala wa sheria. “Historia yetu ni sehemu ya mchango wetu kwa jumuiya ya kimataifa katika kukuza amani, utulivu na maendeleo.”

Amesema hayo Jumatano, Juni 26, 2024 wakati wa uzinduzi wa vitabu viwili vya historia ya bunge katika ukumbi wa Pius Msekwa, Jijini Dodoma.Vitabu vilivyozinduliwa ni Kitabu cha Historia ya Bunge kutoka 1926-2024 na Wabunge wa Tanzania na nafasi zao kuanzia mwaka 1965-2023

“Kumbukumbu za historia ya Bunge zinaweza kuchochea utafiti wa kitaaluma na maendeleo ya nadharia za kisiasa na utawala. Watafiti wanaweza kutumia taarifa hizi kujenga ufahamu mpya na kupendekeza mifumo bora ya kisiasa.”

Kwa upande wake Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amepongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa sehemu ya maono ya bunge ikiwemo kuridhia kulikabidhi bunge maeneo yote yanayozunguka jengo la bunge.

“Tunatarajia kujenga makumbusho ya bunge ambayo yatakuwa ni makubwa kwa nchi nzima ili mtu anapokuja bungeni apate historia ambayo tumeipitia kama nchi lakini pia historia ya bunge letu”

Previous articleRC-MTANDA AIPONGEZA MSD KWA MAGEUZI YA KIUTENDAJI
Next articleNHC KUANZISHA MKOA MPYA WA URAFIKI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here