Home LOCAL SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI MTWARA YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA, MATUMIZI YA...

SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI MTWARA YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA, MATUMIZI YA GESI ASILIA

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiwa katika ziara, Shule yaSekondari Ufundi Mtwara
 
Ikiwa ni Moja ya taasisi inayotumia nishati ya gesi asilia kupikia mkoani Mtwara , Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara inafurahia uwepo wa nishati hiyo kwani licha ya kuokoa pesa nyingi pia imesaidia kutunza mazingira ya shule hiyo kuwa masafi wakati wote huku ikielezwa kuwa hata ratiba za shule kwa sasa zinaenda vizuri kwani chakula kinapikwa na kuiva kwa wakati.
 
Hayo yameelezwa wakati ya ziara ya Wajumbe wa Bodi ya TPDC walipotembelea Shuleni hapo Juni 13, 2024. 
 
Akiongea katika ziara hiyo Makamu Mkuu wa shule Mwl. Bwire Babi alisema “Kabla ya matumizi ya gesi asilia shule tulikuwa tunatumia milioni Sita hadi milioni Saba kila mwezi kwa ajili ya kununua kuni na mkaa lakini tangu kuanza matumizi ya gesi asilia mwaka 2020 kwa mwezi shule inatumia kiasi cha Tsh 1,500,000 hadi 1,600,000, tumepata unafuu mkubwa na tunashukuru serikali na TPDC kwa kutuletea gesi hii’’.
 
 
Aidha, Bwire aliongeza kuwa nyumba za waalimu 31 shuleni hapo nazo zimeunganishwa na mtandao wa gesi asilia ya kupikia hali inayoleta unafuu mkubwa wa nishati.
 
“Nilikuwa natumia hadi 190,000 ikiwa ni gharama ya mkaa na gesi ya mitungi kupikia nyumbani kwangu lakini matumizi haya ya gesi asilia natumia Tsh 30,000 tu kwa mwezi’’ ,aliongea Mwl. Bwire
Makamu Mkuu wa Shule ya Ufundi Mtwara Mwl.Bwire akitoa ufafanuzi wa matumizi ya gesi asilia shuleni hapo kwa Wajumbe wa Bodi ya TPDC
 
Kwa upande wake Mhandisi Samweli Charles alieleza kazi kubwa inayofanywa na TPDC katika kuunganisha Mtwara na mtandao wa gesi asilia kwa matumizi ya viwandani, majumbani na kwenye taasisi.
 
‘‘Hadi sasa nyumba 425 zimeunganishwa na mtandao wa gesi asilia ya kupikia , taasisi nne ambazo ni Shule ya ufundi Mtwara, Chuo cha ualimu Mtwara, Chuo cha ualimu ufundi Mtwara, gereza la Lilungu pamoja na kiwanda cha Saruji cha Dangote , alieleza’’ Mhandisi Charles
Mhandisi Samwel Charles akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC walipotembelea nyumba zinazotumia gesi asilia katika Shule ya Sekondari Ufundi Mtwara, Juni 13, 2024

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here