Home LOCAL SERIKALI YAMUITIKIA MTATURU BUNGENI

SERIKALI YAMUITIKIA MTATURU BUNGENI

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itapeleka fedha kwa ajili ya ukarabati wa Shule Kongwe zilizopo katika Jimbo lake.

Mtaturu ameuliza swali hilo Juni 28,Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu,“ Mh Spika,Shule za Dung’unyi na Kinyamwandyo katika Jimbo la Singida Mashariki ni shule kongwe na zimechakaa,Je ni lini serikali italeta fedha kwa ajili ya kuzikarabati shule hizo,?”.amehoji Mtaturu.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Zainabu Katimba amesema serikali imekuwa ikifanya ukarabati katika shule zote kongwe nchini na tayari imeanza kuhudumia maeneo mbalimbali.

“Na wewe Mh Mbunge nikuhakikishie kuwa,katika jimbo lako kwa sababu kuna shule hizi chakavu fedha zitaletwa kwa ajili ya kuhakikisha miundombinu inaboreshwa na shule zako zinakarabatiwa,”.amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here