Home LOCAL RAIS SAMIA NA RAIS UMARO EMBALO WASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA...

RAIS SAMIA NA RAIS UMARO EMBALO WASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA USHIRIKIANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akitia saini kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira akitia saini kwa upande wa nchi yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.

Previous articleNAIBU WAZIRI KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA FCC MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Next articleTANZANIA NA GUINEA BISSAU ZAKUBALIANA KUKUZA USHIRIKIANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here