Home LOCAL RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA HAKI ZA RAIA KWA MUJIBU WA KATIBA

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA HAKI ZA RAIA KWA MUJIBU WA KATIBA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Hafla ya upokeaji wa Taarifa hiyo imefanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi katika ngazi zote kuendelea kusimamia haki za raia kama zilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa chachu ya mabadiliko chanya kifikra na kimtazamo.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika hafla ya kupokea Ripoti ya Kamati ya Kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Kuangalia Jinai Nchini iliyofanyika Ikulu, Chamwino.

Aidha, Rais Samia ametoa rai kwa Viongozi kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na Tume na kuhamasisha mabadiliko hayo kwa wananchi wanaowaongoza kwa lengo la kujenga upya ili kuimarisha utendaji unaozingatia misingi ya utawala bora.

Vile vile, Rais Samia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutekeleza mamlaka yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na mipaka ya mamlaka hayo.Rais Samia pia amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha inalinda na kuimarisha misingi ya utu, usawa, haki na uongozi bora hapa nchini.Ili kujenga uelewa wa pamoja wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, Rais Samia amewataka Makatibu Wakuu Viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuandaa warsha kwa Viongozi wa Seriikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sharifa B. NyangaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here