DAR ES SALAAM
Rais Samia amevitaka vyombo vya habari kuhamasisha kupokea ujuzi mpya, taarifa za maendeleo ya kiteknolojia katika sekta za uzalishaji na maendeleo ya jamii, vifichue maovu na kutowajibika kunakofanywa na Watumishi na Watendaji wa Serikali, vinatoa mrejesho wa hisia na mtazamo wa wananchi kwa Serikali yao, na kwa ujumla, vinafanya kazi ya kuelimisha na kukuza demokrasia.
Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa masuala haya ndiyo yanayoifanya Serikali kujenga na kuimarisha uhusiano mwema na vyombo vya habari.
Vyombo vya habari sio mshindani wa Serikali bali ni mdau na mshiriki muhimu katika yanayotendwa na Serikali hivyo, Serikali itaendelea kuweka mifumo mizuri ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi, katika kuimarisha uhuru na
mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum kuhusu Kutathmini hali ya Utendaji na Uchumi kwenye Vyombo vya Habari Tanzania Bara kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwandishi Mbobevu Tido Mhando wakati wa Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Baadhi ya Wanahabari Wabobevu wakiwa kwenye Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, Maafisa Habari wa Serikali pamoja na Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Baadhi ya Maafisa Habari kutoka Serikalini, Taasisi mbalimbali za Serikali wakiwa kwenye Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.
Wadau mbalimbali wa Habari, Wanafunzi wa Tasnia ya Habari pamoja na Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2024.