Home LOCAL RAIS SAMIA ASHIRIKI  MKUTANO MAALUM WA  WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA...

RAIS SAMIA ASHIRIKI  MKUTANO MAALUM WA  WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHIRIKI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia majadiliano wakati aliposhiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024.  Mkutano huo umempitisha Veronica Mueni Nduva (Raia wa Kenya) kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo. Bi. Nduva ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa EAC. Marais hao wamekubaliana kufanyike Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Mtangamano kujadili masuala ya amani, ulinzi na usalama pamoja na changamoto zingine zinazoikabili EAC ili kuwasilisha ripoti hiyo kwenye Kikao kijacho cha Wakuu wa Nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini mazungumzo wakati aliposhiriki Mkutano Maalum wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Dar es Salaam tarehe 07 Juni, 2024. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa EAC Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit. Viongozi wengine walioshiriki katika Mkutano huo ni Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, Rais wa Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Musalia Mudavadi na Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Prosper Bazombanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here