Home LOCAL NOSING KIMEREI AMEWATAKA UWT WASINYWE SUMU CCM ISHIKE DOLA

NOSING KIMEREI AMEWATAKA UWT WASINYWE SUMU CCM ISHIKE DOLA

NA: HERI SHAABAN(ILALA)

MWENYEKITI wa Umoja wanawake UWT kata ya Kivule NOSING KIMEREI, amewataka UWT wasinywe sumu badala yake amewataka uwt kuakikisha ccm inashika dola katika chaguzi zake ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani 2025.

Mwenyekiti NOSING KIMEREI alisema hayo katika mkutano wa umoja wanawake UWT Tawi la Mji Mwema Kivule Wilayani Ilala mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka.

“Wanawake wezangu wa uwt sumu aijaribiwi hivyo tusikubali kutawaliwa na wapinzani tuakikishe ccm ina shika dola wanawake UWT jeshi kubwa ambalo linaokoa Chama na Taifa katika shughuli mbalimbali za chama na Serikali uchaguzi wa Serikali za mtaa unaanza Mwezi Julai kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura uweze kupata haki ya kupiga kura” alisema KIMEREI.

Mwenyekiti KIMEREI alisema mwezi Julai mwaka huu Filimbi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa inaanza kwa kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura hivyo akiwaomba wanawake wa UWT kivule kuamasisha wanawake na watoto wao waliofikisha miaka 18 kushiriki kujiandikisha ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika eneo ambalo wanaishi.

Aliwataka wanawake kutoa watoto wao ndani waliotimiza miaka 18 na kujenga umoja na mshikamano katika chama cha Mapinduzi CCM pamoja na jumuiya zake.

KATIBU wa umoja wanawake UWT Mji Mwema Kivule Sarah Isesha alisema tawi la UWT Mji Mwema lina wanawake wa UWT 260 wanachama wa ccm 270 kati yao wenye kadi za mpiga kura 143 na wenye namba za NIDA 140 mikakati yao kuongeza wanachama kufikia 500 .

Katibu Sarah alisema mikakati yao mingine uwt Mji Mwema kwa kuongeza wanachama na kusajili katika mfumo wa kadi za kisasa la electronic .

Akizungumzia changamoto za Tawi la UWT Mji Mwema miundombinu ya Barabara pamoja na Mkopo ya Serikali vikundi vya wanawake wa eneo hilo mikopo aijawafikia.

Mwisho
Habari mawasiliano
0784 496 586
0769 822325

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here