Home BUSINESS NHC KUANZISHA MKOA MPYA WA URAFIKI

NHC KUANZISHA MKOA MPYA WA URAFIKI

DAR ES SALAAM 

Katika juhudi za kuimarisha ufanisi na kuchochea maendeleo katika eneo la Urafiki, Ubungo Jijini Dar es Salaam, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepanga kuanzisha mkoa mpya wa kiutendaji wa Urafiki.

Hatua hii imetangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah, wakati akitoa taarifa kwa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo inayofanya ziara katika miradi mbalimbali kufahamu hatua za utekelezaji na changamoto.

Mkoa huu mpya wa kiutendaji unalenga kuongeza uratibu bora wa shughuli za maendeleo na huduma kwa jamii katika eneo la Urafiki.

Kulingana na Hamad Abdallah, lengo la kuanzisha mkoa huu ni kuwezesha utoaji wa huduma bora za makazi na miundombinu muhimu kwa wakazi wa eneo hilo, huku pia kukuza fursa za kiuchumi na kijamii.

Urafiki ni moja kati ya maeneo yenye ukuaji wa haraka Jijini Dar es Salaam, na kuanzishwa kwa mkoa mpya wa kiutendaji kunatarajiwa kuongeza usimamizi thabiti na ufanisi katika utoaji wa huduma za maendeleo ya jamii na miundombinu ya makazi.

Mpango huu unakusudia pia kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wakazi wa Urafiki kwa kuimarisha mifumo ya utawala na usimamizi.

Kwa ujumla, hatua hii inaonyesha dhamira ya NHC katika kuhakikisha maendeleo endelevu na ustawi wa jamii katika eneo la Urafiki, na inatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa wenyeji wa eneo hilo na jamii kwa ujumla.

Akitoa taarifa fupi ya eneo la Urafiki, Mkurugenzi wa Usimamizi Miliki, Elias Msese amesema eneo hilo lina jumla ya Units 399 majengo ya biashara 6, makazi ya wataalamu 32, shule ya msingi, retail shop 32, maghala 31, yard za magari 10, gereji 4, kituo cha mafuta kimoja, sehemu za kuosha magari tatu. Industrial park.
Kuna viframe vidogo vidogo na makontena.

Amesema kwa kuanzia Shirika linaweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja kwa mwezi na kiasi hicho kitaongezeka kadri maboresho yanavyofanyika.

Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Sophia Kongela amepongeza hatua zote muhimu zilizopigwa baada ya makabidhiano na kutaka Shirika kufanya hatua za haraka zaidi ili kuliboresha eneo hilo.

Previous articleWAZIRI MKUU AZINDUA VITABU VYA HISTORIA YA BUNGE
Next articleBODI YA NHC YAFANYA ZIARA MIRADI YA DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here