Home SPORTS NELSON MANDELA FITNESS CLUB YAZINDULIWA KUBORESHA AFYA MAHALA PA KAZI

NELSON MANDELA FITNESS CLUB YAZINDULIWA KUBORESHA AFYA MAHALA PA KAZI

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imezindua Nelson Mandela Fitness Club yenye lengo la kuboresha afya za wafanyakazi, wanafunzi na jamii inayozunguka katika kujikinga na magonjwa yasiyoyakuambukizwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na Ubunifu Prof Anthony Mshandete Juni 1, 2024 Kampusi ya Tengeru Arusha.

” Kupitia Nelson Mandela Fitness Club tutaongeza tija , ufanisi na kuondoa msongo wa mawazo kwa wanajumuiya ya Nelson Mandela ambao ni wanafunzi, wafanyakazi na Wanajamii kwa ujumla” amesema Mshandete.

Ameongeza kuwa, Nelson Mandela Fitness klabu ni maandalizi ya Nelson Mandela Marathon itakayofanyika septemba 21, 2024 yenye lengo la kuchangia watoto wa kike kujiunga masomo ya elimu ya juu katika nyanja ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Hisabati.

Naye Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanafunzi Bi. Analyce Ichwekeleza ameeleza kuwa, lengo la kuanzishwa kwa Klabu hiyo ni kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Nelson Mandela kushirikiana katika michezo na kuimarisha afya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here