NAIBU Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa ameielekeza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti ya Madini Tanzania (GST),kwenda kufanya utafiti wa awali katika Kata ya Kikio iliyopo Jimbo la Singida Mashariki ili kubaini uwepo wa madini ya chumvi katika eneo hilo.
Maelekezo ya Dkt.Kiruswa yametolewa Juni 4,2024,kufuatia swali la Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu aliyeomba serikali iboreshe viwanda ili kuvutia uwekezaji kuweza kuwekeza katika eneo hilo ambalo ni Bonde lenye chumvi nyingi lakini halijawahi kufanyiwa kazi.
“Kata ya Kikio katika Jimbo la Singida Mashariki ni Bonde lenye chumvi nyingi lakini haijawahi kufanyiwa kazi kwa maana ya vikundi,naomba Wizara itusaidie kuboresha viwanda na kuweza kuvutia wawekezaji katika eneo hilo,”.ameomba.
Akijibu ombi hilo Dkt.Kiruswa amesema GST iende ikafanye utafiti wa awali katika eneo hilo.
“Mh Spika,kwa unyenyekevu mkubwa napokea ombi hilo,na niielekeze GST iende ikafanye utafiti wa awali ili tuweze kuendelea na kutafiti zaidi kuhusu chumvi katika eneo hilo,”.amesema.
[6/5, 10:46 AM] Alex Sonna: MTATURU AIOMBA SERIKALI KUSAIDIA VIWANDA VYA CHUMVI KIKIO.