Home LOCAL MRADI WA HEET KUBORESHA MAABARA ZA NELSON MANDELA

MRADI WA HEET KUBORESHA MAABARA ZA NELSON MANDELA

:

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) akiweka saini ya Makubaliano Mkataba wa vifaa vya maabara vyenye Thamani ya Bilioni 4.3 na Mzabuni Bw. Thomas Elisa Mwasikili (kulia) kutoka Kampuni ya Evolve ya Jijini Dar es Salaam Juni 19, 2024.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) akiweka saini ya Makubaliano Mkataba wa vifaa vya maabara vyenye Thamani ya Bilioni 2.7 na Mzabuni Meneja Bw.Charles Fubusa (kulia) kutoka Kampuni ya Afrika Biosystem Juni 19, 2024

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) wakibadilishana mikataba wa makubaliano wa vifaa vya Maabara vyenye Thamani ya Bilioni 4.3 mara baada ya kusaini na Mzabuni Bw. Thomas Elisa Mwasikili (kulia) kutoka Kampuni ya Evolve ya Jijini Dar es Salaam Juni 19, 2024.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( kushoto) wakionyesha Makubaliano Mkataba wa vifaa vya maabara vyenye Thamani ya Bilioni 2.7 na Mzabuni Meneja Bw.Charles Fubusa (kulia) kutoka Kampuni ya Afrika Biosystem mara baada ya kuweka saini Juni 19, 2024 jijini Arusha.

Na.Mwandishi Wetu
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imesaini mkataba na wazabuni wawili wa usambazaji wa vifaa vya maabara wenye thamani ya Bilioni 7 kwa ajili ya kuboresha maabara kukidhi viwango vya Kimataifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mikataba hiyo, Juni 19, 2024 katika Kampasi ya Tengeru Arusha , Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, vifaa hivyo vitaimarisha utafiti na ubunifu wakati wa uchakataji wa sampuli na uchunguzi wa vihatarishi ili kuzalisha bidhaa bora kwa watumiaji vyenye viwango vya Kimataifa zitakazotumika ndani na nje ya nchi.

“Kiasi kikubwa cha pesa zilizotolewa na Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Elimu ya Juu (HEET PROJECT) tumeelekeza kwenye manunuzi ya vifaa vya maabara vyenye hadhi ya kimataifa ili kuwa na maabara zitakazoweza kuleta mabadiliko ya viwanda nchini na kusaidia uzalishaji wa mazao na bidhaa zenye ubora kimataifa” amesema Prof. Kipanyula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Evolve ya Jijini Dar es Salaam Bw. Thomas Elisa Mwasikili amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuziwezesha taasisi mbalimbali kupitia mradi wa HEET na kwa kuaminiwa na taasisi ya NM-AIST kufanya kazi ya uzabuni yenye Thamani ya shilingi bilioni 4.3 na kuahidi kukamilisha kwa muda kama mkataba unavyoelekeza.

Naye Meneja wa Kampuni ya Afrika Biosystem Bw. Charles Fubusa aliyesaini mkataba wa zabuni wenye thamani ya Bilioni 2.7 ameeleza kuwa atasimamia, kutekeleza na kufanikisha yaliyo ndani ya mkataba kwa wakati .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here