Home LOCAL MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA AONGOZA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU

MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA AONGOZA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU

 

John Francis Haule akichangia damu salama

**

Katika viwanja vya soko kuu Arusha siku ya Juni 28, 2024 kumeendeshwa zoezi la uchangiaji Damu salama kwa hiari.

Zoezi hilo limeongozwa na mkuu wa soko kuu la Arusha ndg. John Francis Haule kwa kushirikiana na watumishi wa jiji la Arusha na wafanya biashara.


Dhumuni na shabaha  kuu ya zoezi hili ni kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya uchngiaji damu na jitihada zinazo fanywa na serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais wa jamuhuri ya Muungnaano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wote wa chama na serikali katika  kuimarisha  na kuboresha miundombinu ya sekta ya afya.

Hili limedhihirika kwa vitendo katika ujenzi wa zahanati,vituo vya afya,hospital za wilaya mikoa na hata mageuzi makubwa katika hospitali ya taifa Muhimbili hivyo kwa jitihada hizo zote nasi tumeona hatuna budi kuunga  mkono juhudi hizo kwa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji.

 

Pia hata bajeti  ya Wizara ya Afya ya 2024/2025 ni kubwa. Huu ni uthibitisho tosha kuwa serikali imeweka jitihada kubwa za kuhakikisha sekta ya afya inakuwa imara  kwa miundombinu na hata vifaa tiba vya kisasa.

 

Pia tumeona hii programu ya   “Madaktari Bingwa Wa Samia” hawa madaktari bingwa wamesambaa katika hospitali zote za wilaya nchi nzima wa kitoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa hii haija waai tokea tangu tupate  uhuru  imekuwa ni programu mwokozi hasa kwa wagonjwa ambao hawana kipato cha kutosha kufika katika hospitali za kanda na za mikoa hivyo hili ni jambo jema na lakuungwa mkono na kila Mtanzania na hii imedhihirisha Dhamira ya dhati ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt.  Samia Suluhu Hassan Katika kujali na kuimarisha  Afya za wananchi.

 

Pia hapa Arusha tunaona  huduma za afya zikifanyika hapa uwanja wa shekhe amri abed madaktari wa mekita kambi wakitoa huduma za vipimo na matibabu bure kwa wanannchi program iliyo buniwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mh.Paul Christian Makonda hii pia ina akisi namna viongozi waandamizi wa serikali wanavyo tafsiri dhamira ya thati ya Mkuu nchi katika kutoa huduma za afya kwa jamii hili nijambo la kuungwa mkono na kila mwanchi hasa wale wenye mlengo wa kizakendo ,hivyo nasi hatuna budi ya kuunga mkono kwa kile ambacho tunaweza fanya hasa kwa kujitolea  kuchangia damu ili kuweza kuokoa maisha ya wahitaji.

 

Damu mahitaji yake ni makubwa sana na upatikanaji wake ni wa asili maana kwamba hakuna kiwanda kinacho chakata damu dhidi ya kutoka kwa binadamu hivyo  na toa wito kwa wa Tanzania tujenge desturi ya kuchangia damu kwa  hiari. Pia na shauri wale tuliopewa dhamana ya kuongoza ama kusimamia maeneo yenye  mkusanyiko wa watu wengi  tutumie hio fursa kuhamasisha jamii kuwa na desturi  ya kuchangia damu, mfano vyuoni,kwenye makongamano ya dini. Hata viwanj a vya mpira. Mfano tume shudia 2023 Team ya yanga pale jangwani wa nachama wake walichangia  Damu na hata Mh. Ummy Mwalimu Waziri wa afya aliwapongeza sana, hivyo na wengine tuige mfano huo mzuri ulio onyeshwa na team ya yanga kwa kufanya jambo la kiutu na la kizalendo.

 

PONGEZI KWA SERIKALI

Akihitimisha zoezi hilo Ndg John  Francis Haule  ambaye ni mkuu wa soko kuu la Arusha    (market master)  ametoa pongezi kwa serikali  na kwa  Chama Cha Mapinduzi kwa kuhakikisha Huduma za afya zina mfikia kila mtanzania hata yule alioko kijijini.

Nahimiza  wa Tanzania tujitahidi kuwa wazalendo wa kweli kwa kuunga mkono serikali hasa katika kampeni hii ya kitaifa ya kuhamasisha kila mtanznia mwenye sifa za kuchangia damu kufanya ivvo ili kuokoa maisha ya wahitaji nahii yote ni kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

 

 

WALIOCHANGIA DAMU WANENA

 

Akizungumza baada ya kuchangia Damu ndg  Mallya ambaye ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara  amebainisha kuwa suala hili la kuchangia damu ni suala zuri la kiutu na la kibinadamu hivyo watu tujenge desturi ya kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha kama isemavyo kauli mbiu ya wizaara ya afya “Changia Damu Uokoe Maisha”.

 

Naye kijana James Masue baada ya kuchangia damu amebainisha kuwa jambo ili liwe endelevu kwa kuwa lina tija kubwa kwa wana nchi, Pia Jacqline Galle ambaye ni mtumishi wa jiji la Arusha amebainisha kuwa mahitaji ya damu ni makubwa hasa kwa akina mama  na majeruhi wa ajali  hivyo hamasa hii iwe endelevu na hata katika mitaala ya elimu kuwezesha  watu kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa kuchangia damu.

 

Naye Humprey Mwarija  mshiriki na mtumishi wa jiji la Arusha amebainisha kuwa  maumivu tunayoyapata wakati wa kutoa damu ni kidogo na ni ya muda kulilo huzuni na maumivu ya kuondokewa na ndg kwa sababu tu ya kukosekana kwa Damu. Hivyo wa Tanzania ifike wakati vifo vinavyo sababishwa na ukosefu wa Damu tuvi fute nahi inawezekana tu kwa kila mwenye afya njema kuchangia Damu ilikila hospitali iwe na akiba ya kutosha ya Damu ili isaidie wakati wa dharura na hili ni jambo linaweekana kwa kila mmoja wetu kujitoa kwa kuchangia damu.

 

 

MRATIBU WA MPANGO WA DAMU SALAMA KITAIFA  ANENA

 

Akitoa elimu kabla ya kuanza kwa zoeezi hilo la uchangiaji damu  mratibu wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha watu kuchangia damu

Ameainisha kuwa sifa za mtu kuchangia damu ina takiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 65. Awe na afya njema  yaani asiwe na maradhi ya kudumu kama vile kisukari,BP. Na magonjwa ya kuambukiza na akina mama wanao nyonyesha na waja wazito hawa ruhusiwi kuchangia damu.

 

 

Hii imeendaliwa na NDG. JOHN FRANCIS HAULE

MKUU WA SOKO KUU LA ARUSHA.

SIMU 0756717987 au 0711993907

Email : haulej46@yahoo.com

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here