Home LOCAL MBUNGE MTATURU AWASHA MOTO BUNGENI

MBUNGE MTATURU AWASHA MOTO BUNGENI

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini kituo cha afya cha Ntuntu kilichopo jimboni kwake kitaanza kufanya kazi.

Mtaturu ameuliza swali hilo Juni 10,2024,Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.

“Mh Mwenyekiti,kituo cha afya cha Ntuntu kilitengewa Sh Milioni 500 huu unaenda mwaka wa pili lakini hakijaanza kufanya kazi pamoja na kwamba tulipata fedha kwa awamu tofauti,

“Nataka nijue ni lini kituo hicho kitaanza kufanya kazi kwa sababu wananchi wanakisubiri kwa muda mrefu na ni kituo cha mkakati,”.amehoji.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Dkt.Festo Dugange amekiri kuwa ni kweli kuna baadhi ya vituo vya afya ambavyo vilijengwa na kukamilika lakini bado havijaanza kutoa huduma.

“Naomba niwakumbushe na kuwasisitiza wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kikiwemo na kituo cha afya cha Ntuntu, baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupeleka fedha na kukamilika kwa vituo,matarajio ya wananchi ni kuanza kupata huduma kupitia vituo hivyo,

“Serikali haitakuwa tayari kuona kituo kimekamilika lakini hakitoi huduma na wananchi wanahitaji huduma,naomba nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi kuhakikisha ndani ya miezi miwili kituo hicho kianze kufanya kazi na wananchi wapate huduma,”.ameelekeza.

Previous articleNAULI MPYA ZA ABIRIA KWA DARAJA LA KAWAIDA – TRENI YA KISASA (SGR)
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 11-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here